Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kutokana na changamoto hiyo amesema katika kukabiliana na nayo tayari DAWASA wapo katika hatua za mwisho kukamilisha mazungumzo na Serikali ya Korea ili kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa ambao utaleta suluhu katika maeneo ya katikati ya Jiji hususani Kariakoo na Buguruni.
"Kwa sasa hivi tuna mradi mkubwa, ambapo tupo katika hatua za mwisho kumpata Mkandarasi kwa ajili ya utekelezaji hususani eneo la katikati ya Jiji ambako ni maeneo ya Buguruni na Kariakoo," amasema Bwire.
Amesema hatua ya mazungumzo inaendelea vizuri na kwamba kufikia Januari 2025, Mkandarasi tayari atakuwa ameanza utekelezaji wa mradi huo.
Hayo ameyasema Septemba 14, 2024 ambapo Waziri wa Maji, Juma Aweso pamoja na Mtendaji huyo na Watendaji wengine wa DAWASA wamengoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Serikali kupitia Dawasa.
Ambapo kati ya miradi iliyotembelewa ni mradi wa kukusanya majitaka ambao unajengwa eneo la Mbezi Beach Dar es Salaam ukuwa na thamani ya fedha Tsh. Bilioni 132.
DAWASA wakati wakifafanua utekelezwaji wa mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Belgian Construction, wameeleza kuwa mradi umefikia asilimia 57 ya utekelezwaji na kwamba mabomba zaidi ya 100 yatatandazwa katika mradi huo, ambapo suala hilo tayari limeanza.
Ambao wamesema kuwa unalenga kupunguza changamoto za majitaka katika Kata ya Mbezi beach, Mbezi juu, Kunduchi pamoja na maeneo mengine ya karibu.
Pia, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga (Mb), kwa niaba ya Kamati, amesema wamefika kukagua baadhi ya miradi ya majitaka ambayo inatekelezwa Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema Kamati hiyo iliagiza Miji yote inayokua iwe na mifumo rafiki ya kisasa ya majitaka ili kulinda mazingira sambamba na kwenda na kasi ya ukuaji wa miji.
Amesema wameona jitihada zinazoendelea ili kukabili changamoto kulingana na maelezo yaliyotolewa awali na Kamati hiyo.
"Sasa hivi (DAWASA) uwezo wao wa kukusanya uchafu haufikii asilimia 50, kwahiyo tuliomba waongeze kasi, kwahiyo kikubwa tulichokiona, kwanza tumeona kazi zikiendelea vizuri. Lakini cha ziada ambacho tumekiona kwenye mipango ya majitaka ni pamoja na ule uchafu ambao unatoka kwenye mfumo wa majitaka unazalishwa kuwa mbolea, lakini tumeona sehemu nyingine tena uchafu ule wanauzalisha kuwa gesi kwa ajili ya matumizi," amesema Kiswaga.
Aidha, Waziri wa Maji Juma Aweso amesisitiza maelekezo ambayo ameyatoa kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuhusu Wizara kubadilika kiutendaji ili kuongeza kasi na kufanikisha miradi inayotekelezwa na inayokusudiwa kutekelezwa kukamilika kwa wakati, akidai kuwa uwezeshaji upo.
Ambapo amesema kama pesa ya utekelezaji wa miradi hiyo ipo kunakuwa hakuna sababu inayoweka kikwazo kwa shughuli za utekelezaji wa mradi kufanyika usiku na mchana ili kuwezesha wananchi kunufaika na miradi hiyo kwa wakati.
"Na hili ni elekezo nimelitoa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, lazima kama Wizara tubadilike katika mfumo wa utendaji kazi, ipo miradi mikubwa ambayo pesa zake zipo kwahiyo hakuna sababu ya kufanya tu mchana, ni wakati muafaka pia utendaji kazi kufanyika hadi husiku ili miradi iweze kukamilika kwa wakati," amesema Aweso.
Pia soma:
Kariakoo kuna chemba zinatema maji machafu na kuhatarisha afya za Watu, Viongozi wapo kimya