boyson onlye
JF-Expert Member
- Sep 13, 2015
- 1,108
- 1,397
Habari wakuu,
Nina miaka kadhaa katika jiji hili la Dar es salaam, na wengine wote wanaoishi katika jiji hili ni mashahidi,
Kila nyumba ina vifaa vingi vya kutunzia maji, iwe ndoo, jaba au tank na kuna wakati unakuta maji yote uliyotunza yameisha ndanj na maji hayatoki, hasa kipindi hiki ambacho mvua si za kutosha na hata kipindi cha mvua haijawai kutokea maji yametoka mwezi mzima mfululizo bila kukatika.
Kwa hiki kipindi maeneo kadhaa ya Dar es salaam yamekosa maji kabisa na mifumo ya maji ipo na DAWASCO hawasemi chochote wala kutoa tahadhali yoyote.
Je, miaka 60 ya uhuru Dawasco haina mpango mkakati wa kusambaza maji kwa uhakika katika jiji hili la Biashara, nini sababu ya kutotoa huduma ya maji kwa uhakika, kama Dawasco imeshindwa kwa nini isipewe kampuni Binafsi kuendesha shirika hili kama walivyo fanya Bandari.