KERO DAWASA, wakazi wa Kimara Korogwe njia ya Mji Mpya kuelekea KAM College hatuna maji wiki ya pili sasa

KERO DAWASA, wakazi wa Kimara Korogwe njia ya Mji Mpya kuelekea KAM College hatuna maji wiki ya pili sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Wakazi wa Kimara Korogwe upande wa njia inayopita Mji Mpya kuelekea KAM College tunahangaika kwa uhaba wa maji, hali hii inaleta usumbufu mkubwa kwani kinachotokea sasa siyo utaratibu wa kawaida uliozoeleka ambapo awali, maji yalikuwa yanatoka kwa mgawo mara 2 kwa wiki, siku ya Jumanne alfajiri na siku ya Alhamisi alfajiri.

Kinachosikitisha zaidi, mitaa ya jirani inapata maji ya kutosha, umbali usiozidi mita 100 kutoka nyuma ya mwisho kuelekea mtaa wetu ambako hakuna kabisa maji.

Tunajiuliza, DAWASA mmepatwa na shida gani? Kwanini maji yamegeuka kuwa anasa wakati ni hitaji muhimu la binadamu? Kwanini hamtoi taarifa yoyote juu ya uwepo wa changamoto hii ili watu wajue nini cha kufanya?

Hii siyo sawa na haikubaliki. Tunajaribi kutumia lugha ya kiungwana ili mtuelewe, haiwezekani huduma ya msingi kabisa hata baada ya miaka 60 ya Uhuru tunashindwa kuipata kwa uhakika. Jitafakarini!
 
Back
Top Bottom