DAWASA wanatoa wapi maji wanayowauzia wenye magari ili waje kutuuzia mtaani?

DAWASA wanatoa wapi maji wanayowauzia wenye magari ili waje kutuuzia mtaani?

Ni katika kuhangaika kupata maji leo asubuhi nikampanga kijana anaesambaza maji kwa kutumia gari akiniambia saa mbili asubuhi atakuwa ameshaleta hayo maji.

Saa mbili na nusu nampigia kujua kama anakuja au niendelee kutafuta njia nyingine ya kupata huduma hii muhimu, akaniambia anasubiri dawasco wafungue ili aweze kujaza maji kwenye tank lake.

Saa nne alikuwa ameshafika, nikamuuliza inakuwaje dawasco wanauza maji wakati huku mtaani hatuna maji? Kijana akaniambia Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. 'kwahyo haya maji syo mgao?' nilimuuliza, 'inawezekana lakini syo mara zote' alinijibu.

Dawasco ubungo acheni hiyo michezo, mnatuumiza sana wananchi wa hali ya chini, imagine Lita 3000 nanunua kwa sh. 50,000 kweli?
Dawasco ubungo na kibamba wanashirikiana na wenye canters za kuuza maji,huwezi kusikia shida ya maji mara kwa mara kigamboni sababu hakuna vile vicanter
 
Kuna wenye Tamaa Kama Mzee Makorere aliekezea maji kwake dili ilichezwa na Mainjinia, mameneja kujumuisha na watu wa supply.
Mainjinia nao wanamiliki visima na wanauza maji hayo ya wizi yaliyotakiwa kufikia watu wakayaelekezea kwao.

Yani Hadi ajaze visima ndio mje kuachiliwa na nyie muokoteze ya njiani.
Hii nchi ni ya kishenzi sana plus tuna viongozi wasiojitambua ndiyo shida inazidi kuongezeka.
 
Maji yamekuwa kero kubwa sana, na waziri yupo anatoa zawadi za ng'ombe na nazi huku wananchi hawana huduma za maji

Hiki chama kimejichokea
Mkuu kama unaweza Mh. Aone haka kauzi tusaidieni. Ubungo ni shida sana maji Tena kipindi chote Cha mwaka mzima. Masika iliyopita maji yalikuwa ya mgao, kuuliza wakasema wanasafisha pipes za maji. Sijui sasahivi watatuambia Nini tukihoji🤔
 
Muda wa bure bado, wana waandaa kwa uchaguzi.

Mkasirikeee mpige kelele,,halafu atajitokeza aseme "Nimeagiza mamlaka zote hakuna mgao wa maji wala umeme" mtapiga makofi na kukenua meno.

Kuanzia mwezi wa 9 mtapata maji hadi ya kumwagilia bustani zenu.

Uchaguzi ukiisha tu, mnarudi mlikotoka.
 
Kuna wenye Tamaa Kama Mzee Makorere aliekezea maji kwake dili ilichezwa na Mainjinia, mameneja kujumuisha na watu wa supply.
Mainjinia nao wanamiliki visima na wanauza maji hayo ya wizi yaliyotakiwa kufikia watu wakayaelekezea kwao.

Yani Hadi ajaze visima ndio mje kuachiliwa na nyie muokoteze ya njiani.
Loh! 😓
 
Rushwa,wenye hivyo vicanter vya kuuza maji wanachangishana kuna fungu linaenda kwa mkurugenzi wa area husika anaamuru maji upande fulani yafungwe mafundi wanaagizwa wabuni tatizo lolote lenye kueleweka maelezo waseme ndiyo shida.

Limetutesa sana Mbezi Makabe hili tatizo hata sasa bado wanafanya michezo hii,ukitoka nyumbani maji hamna ukifika mtaani maji pressure imepasua mabomba yanamwagika barabarani huku hivyo vigari vikitimua vumbi kuuza maji.
Huko makabe msakuzi sjui maji ni shida sana
Uchaguzi ukikaribia ndiyo wataanza kusogezea watu maji

Ova
 
Muda wa bure bado, wana waandaa kwa uchaguzi.

Mkasirikeee mpige kelele,,halafu atajitokeza aseme "Nimeagiza mamlaka zote hakuna mgao wa maji wala umeme" mtapiga makofi na kukenua meno.

Kuanzia mwezi wa 9 mtapata maji hadi ya kumwagilia bustani zenu.

Uchaguzi ukiisha tu, mnarudi mlikotoka.
Na wajinga watashangilia

Ova
 
Dawasco ubungo na kibamba wanashirikiana na wenye canters za kuuza maji,huwezi kusikia shida ya maji mara kwa mara kigamboni sababu hakuna vile vicanter
Vicanter sio vinaenda kwenye shida? Zishatokaga gari Dar kwenda mikoa ya kusini kufanys kazi kama hii
 
Andamaneni hadi hapo dawasco sasa wakuu
 
Kuna mdau alishawahi kusema Ubungo sio sehemu ya kuishi sababu ya uhaba wa maji

Kwa wajuzi wa mambo,kuna nini huko Ubungo hadi wanakutana na hii tabu?
Naishi ubungo maji mbona yanatoka mpka mda huu
 
Ila kuna mtu anawauziaga hao wenye makenta na boza kwake huwaga maji hayakatikagi ni mbibi mjane Mungu kweli hakunyimi yote
 
Naishi ubungo maji mbona yanatoka mpka mda huu
Kwakua wewe ni mwenyeji wa ubungo je kuna shida ya maji maeneno karibu yako hata kama kwako yanatoka?

Binafsi napokaa zamani ng'ambo ya pili umeme ulikua haukatiki ili ng'ambo ya kwetu kukatikanhapa na pale lilikua jambo la kawaida. Wale wengine ilikua ukikatika maeneo yao basi ujue ni tatito kubwa sana limetokea either kanda nzima au nchi nzima
 
Naishi ubungo maji mbona yanatoka mpka mda huu
Mkuu huku makuburi yote, kuanzia makamba sekondari, jeshini, external, garage, kwa mbonde , maduka kumi, mikongeni mpaka karibu na mwananchi kule hakuna maji hata muda huu
 
Back
Top Bottom