Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la kugawa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya Majisafi kwa jumla ya wateja walioomba huduma ndani ya eneo la kihuduma la DAWASA ambalo ni Mikoa ya Pwani na Dar es salaam.
Zoezi hilo limeendelea katika Mikoa ya kihuduma DAWASA Kinyerezi, DAWASA Mapinga, DAWASA Kawe, DAWASA Bagamoyo, DAWASA Mabwepande, DAWASA Tegeta na DAWASA Makongo.
Zoezi hili ni muendelezo wa juhudi za DAWASA za kusogeza huduma ya Majisafi kwa Wananchi wanaopatikana ndani ya eneo lake la kihuduma.
Akizungumza wakati wa zoezi la maunganisho ya wateja wapya wa maji katika Mkoa huo wa kihuduma, Mhandisi wa Miradi wa DAWASA Bagamoyo, Mohammed Ahmad amesema "Zoezi hili limehisusisha utoaji wa vifaa vya maunganisho ya huduma ya majisafi kwa wateja wapatao 70 ambao ni miongoni mwa waliokamilisha kulipia huduma hiyo kwa kipindi kilichopita na sasa wamepata fursa ya kupatiwa vifaa hivyo tayari kuunganishwa na huduma waliyokuwa wanaisubiri kwa hamu kubwa".
Mhandisi Ahmad ameongeza kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo kwa wateja hao ni kuwaunganishia na kusogeza huduma kwa wananchi wa kata za Zinga, Bagamoyo Mjini, Kilomo na Yombo pamoja na kuhakikisha wananchi wote wa Bagamoyo wanapata huduma ya majisafi na salama.
Pia, soma: DOKEZO - DAWASA Kibaha Wamesitisha Huduma ya Kuunganisha Maji kwa Wateja wapya