DAWASCO na maji yenye tope Dar es Salaam

DAWASCO na maji yenye tope Dar es Salaam

BabuFey

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2023
Posts
1,659
Reaction score
2,913
Muda so baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam ukifungua maji ya DAWASCO asubuhi unakutana na tope zito.

Maji haya machafu hayafai kwa lolote, hivyo mtu unamwaga mpaka lita mia moja unayolipia ndio upate masafi.

Kusafisha na kutibu maji kwa kutumia Aluminium sulphate na chlorine siku hizi za kipindupindu sio sayansi ya roketi.

Mnasumbua na message zenu za vitisho vya lipa bili mara tuu mnapo tutumia huku huduma ya hovyo.

Waziri Aweso baada ya kusema "Nani Kama rais Samia" shughulikiwa kero hii.
 
Naomba nikusahihishe Mkuu, Kwasasa hakuna DAWASCO tena hapo Dar Es Salaam isipokuwa pana DAWASA, Mamlaka ya Usambazaji Maji Safi na Taka Dar es Salaam.

Kama Maji yamekuwa na tope, huenda itakuwa kuna Mvua zimenyesha huko kwenye Vyanzo hivyo kupelekea Maji kuchafuka.

Unaweza kuwatembelea ofisini kwao au uwapigie namba ya huduma kwa Mteja kwaajili ya kuripoti.
 
Kwenye ripoti zao wanatuambia Dar es salaam kuna upatikanaji wa Maji safi na salama kwa asilimia 250% nacheka huku nikitabasamu.. 😀
 
Back
Top Bottom