DAWASCO wizi wenu umekithiri sasa

DAWASCO wizi wenu umekithiri sasa

Ngurukia

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2023
Posts
4,407
Reaction score
16,942
DAWASA huu wizi unatosha sasa. Kwa mtindo huu tutaishia kutumia maji ya visima tu.

Kwa miaka takriban minne natumia maji ya DAWASA, familia yangu yote sio ya kushinda nyumbani ikimaanisha kutwa nzima hakuna matumizi ya maji.

Kwa miaka yote hiyo bili yangu ilikuwa haivuki units 4 kwa mwezi.

Ghafla leo asubuhi nakutana na bili kuwa mwezi uliopita sijatumia maji kabisa ikiwa sio kweli na kuwa mwezi huu nimetumia units 23. Ikimaanisha ndani ya wiki 2 nimetumia units 23.

Kubwa na la ajabu zaidi baada ya kwenda kuangalia meter nakuta kumbe wameweka mita mpya bila kunitaarifu, nitakuwa na ithibati gani kuwa hiyo meter ilianza kusoma 0?

DAWASA mmezidi wizi.
Screenshot_20230616-115740_Messages.jpg
 
Unit 0 means siku aliyopita kusoma hamkuwepo nyumbani( kama meter iko ndani)
Na yeye akapekeka report ofisini.

Kama iko nje msomaji hakuja..
 
We kwa mara ya mwisho unakumbuka mita ilisoma unit ngapi? Ni vema kuweka kumbukumbu za meseji wanazotuma. Hapa nadhani ni misunderstanding tu, watakuelewa sio wezi
 
Ipo nje na ndio maana waliweza kuibadilisha bila sisi kujua.
 
We kwa mara ya mwisho unakumbuka mita ilisoma unit ngapi? Ni vema kuweka kumbukumbu za meseji wanazotuma. Hapa nadhani ni misunderstanding tu, watakuelewa sio wezi
Nilikuwa na units 195 kutoka 191 ambayo ilikuwa matumizi ya mwezi uliopita.
 
Hapa nenda ofisini kwao, utapata muongozo mzuri,
1. Kwanini walibadilisha mita?
2. Kwanini hujataarifiwa?
 
Hivi Dawasco na Dawasa ni kitu kilekile? Au Dawasco ndiyo ilibadilishwa ikawa Dawasa. Uwa nachanganya hapa.
 
Hapa nenda ofisini kwao, utapata muongozo mzuri,
1. Kwanini walibadilisha mita?
2. Kwanini hujataarifiwa?
Nimepiga huduma kwa wateja hatimae nimewapata, jibu wanalonipa ni kuwa wanaona kweli kuwa matumizi yangu ni constant (hayavuki units 8) ila itabidi nilipie tu hizo units 23 maana zishaingia kwenye record yao ila wata lodge complaint ya kubadilishiwa mita bila taarifa.

Kwa maana nyingine nikubali kulipia bili ambayo sijaitumia kwa vile tu ishaingia kwenye record yao.
 
Mods naomba muhariri heading iwe DAWASA na si DAWASCO.

DAWASA=DAWASCO=NUWA Ni kitu kimoja mkuu.

Unit 23 kwa Familia moja ni nyingi sana unless uwe unamwagilia gardeni ,miti 24/7.

Mimi natumia unit 5 mpaka 6 kwa mwezi coz si watu wa kushinda home sana.(wastani wa Dumu 8 mpaka 10 kwa siku).
 
Nimepiga huduma kwa wateja hatimae nimewapata, jibu wanalonipa ni kuwa wanaona kweli kuwa matumizi yangu ni constant (hayavuki units 8) ila itabidi nilipie tu hizo units 23 maana zishaingia kwenye record yao ila wata lodge complaint ya kubadilishiwa mita bila taarifa.

Kwa maana nyingine nikubali kulipia bili ambayo sijaitumia kwa vile tu ishaingia kwenye record yao.

Huo ni wizi ,hawa jamaa sijui wakoje ,mimi wakati nafunga maji ilikuja bill 321k wakati wa kuja kulipa kwenye control number ikaja 389k.
 
DAWASA ni moja kati ya mashirika yenye ubabaifu mkubwa mno. Kwa macho yangu nilishawahi muona msoma mita amekaa chini ya mti anaandika units za uongo. Alichokuwa anafanya ni madirio ya record ya mwezi uliopita wa kila mita kwenye huo mtaa na kujaza kwenye karatasi yake ikimaanisha hizo ndio bill wanazotumiwa wateja.
 
DAWASA=DAWASCO=NUWA Ni kitu kimoja mkuu.

Unit 23 kwa Familia moja ni nyingi sana unless uwe unamwagilia gardeni ,miti 24/7.

Mimi natumia unit 5 mpaka 6 kwa mwezi coz si watu wa kushinda home sana.(wastani wa Dumu 8 mpaka 10 kwa siku).
hakuna hata mti wa ushahidi hapo kwangu achilia mbali bustani mkuu.
 
Huo ni wizi ,hawa jamaa sijui wakoje ,mimi wakati nafunga maji ilikuja bill 321k wakati wa kuja kulipa kwenye control number ikaja 389k.
tatizo hakuna sehemu yeyote ya maana mtu anayoweza kwenda kulalamika. Ikiwa mtoa huduma anakujibu kwa wepesi kabisa kuwa lipa tu maana ishasoma unadhani kuna cha maana gani hata huko ofisini kwao mtu ataambiwa?
 
Nimepiga huduma kwa wateja hatimae nimewapata, jibu wanalonipa ni kuwa wanaona kweli kuwa matumizi yangu ni constant (hayavuki units 8) ila itabidi nilipie tu hizo units 23 maana zishaingia kwenye record yao ila wata lodge complaint ya kubadilishiwa mita bila taarifa.

Kwa maana nyingine nikubali kulipia bili ambayo sijaitumia kwa vile tu ishaingia kwenye record yao.
Hilo jibu walilokupa lina ukakasi mno. Fika ofisini kwao na uombe kuongea na manager wao.
 
DAWASA=DAWASCO=NUWA Ni kitu kimoja mkuu.

Unit 23 kwa Familia moja ni nyingi sana unless uwe unamwagilia gardeni ,miti 24/7.

Mimi natumia unit 5 mpaka 6 kwa mwezi coz si watu wa kushinda home sana.(wastani wa Dumu 8 mpaka 10 kwa siku).
Unit 23 ni wastani wa Ndoo 1150
Sawa na Ndoo 40 kila siku
 
Back
Top Bottom