TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi Tanzania, limepata taarifa za watu ambao siyo raia wa Tanzania kuwa wameingia nchini kwa njia zisizo rasmi kwa nia ovu ya kufanya uhalifu ikiwepo vurugu. Watu hao wanajifanya kuwa wanafanya shughuli mbalimbali ikiwepo za bodaboda.
Taarifa zinasema watu hao wapo katika Mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Songwe na Mikoa mingineyo.
Wakati Jeshi la Polisi linaendelea kuwafuatilia ili kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa Sheria, mwananchi yeyote ambaye amempangisha au anaishi na raia yeyote wa kigeni asiyefahamika na anafanya shughuli gani na mienendo yake ni ya kutia mashaka atoe taarifa haraka sana kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Wakuu wa Vituo vya Polisi, Wakuu wa Polisi Wilaya, Makamanda wa Polisi Mikoa au apige simu kupitia namba 0699998899.
Asipotoa taarifa na watu hao wakakutwa nyumbani kwake au eneo lake la biashara hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia wananchi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kuhakikisha Taifa letu linaendelea kuwa salama na lenye amani.
Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania