GE2025 Day 5: Polisi wasema kuna wageni wameingia nchini kuchochea vurugu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Subiri muwashe internet, ushahidi wote utawekwa adharani. Very sad
 
02 November 2025
Dodoma, Tanzania

Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime, ametahadharisha juu ya uwepo wa kikundi cha wageni

Tanzania Police Force Spokesperson DCP David Misime has warned about the presence of a foreign group operating clandestine activities in Tanzania, using motorbikes in the cities and towns to cause ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZWtTNwSDTFE
 
Duh! Ila mkuu mayalla mbona unauliza maswali yakitoto sana , nini shida? anyway legitimacy ya kutawala ni kitendo cha watawaliwa kukubali kutawaliwa na anawatawala, simple as that.
Asante, endelea kunielimisha, hawa watawaliwa wanatumia lugha gani kuonyesha kukubali kutawaliwa na anaye watawala?
Swali , Sa100 anayo hiyo legitimacy? Au anayo kwasababu ya kupewa hiyo 98% hiyo ya mezani?
Ukiisha jibu hapo juu, ndipo nakuja kujibu hili.
P
 
Kwakuwa nakuheshimu sana mkuu mayalla hivyo naona nibusara kama huu mjadala nikaupuuza ili kuepukana na majadiliano yasiyo na afya.
Asante Kriss na Asante kuniheshimu, mambo ya legality na legitimacy ni hoja za kisheria na sio... anyway
Uwe na siku njema
P
 

Wameanza kudpin na kuleta propaganda uchwara. Intelligence zao zinafafa kazi tu kwa Chadema? Iweje watu wengi waingie nchini na wasambae mikoani bila kujua. Wasituletee Uhuni hapa.
 
Ni sheria gani ilitumika katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM?
Karibu, japo mimi sikubaliani na kilichofanywa na CCM kumpitisha mgombea wake,
Thread 'Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa' Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Lakini mkutano wake mkuu una mamlaka ya kufanya chochote hata kuikiuka katiba yake Thread 'Ijue Katiba ya CCM: Malengo ya CCM, Nguvu za CCM, Vikao vya CCM, na Mamlaka ya Mkutano Mkuu wa CCM, Uamuzi Wake ni wa Mwisho!, Final & Conclusive!.' Ijue Katiba ya CCM: Malengo ya CCM, Nguvu za CCM, Vikao vya CCM, na Mamlaka ya Mkutano Mkuu wa CCM, Uamuzi Wake ni wa Mwisho!, Final & Conclusive!.

Chama cha siasa kiko huru kumteua mgombea wake kwa namna yoyote ile kinaona anafaa, ndio maana hata Act Wazalendo kimemuokota Mpina, kikafanyiwa fhulma kubwa.

P
 


Ila brother, wewe katika kung'ata na kupuliza uko vizuri sana.

Nimelisoma hilo bandiko lako, kwa kiasi kikubwa umeonesha mara kadhaa kuwa mchakato haukufuata sheria na kuonya kama kanuni za chama hazikufuatwa, katiba je?

Kuna mambo mengi yaliyo wazi ambayo hayakuwa sawa (mf. utekaji na sasa mauaji ya halaiki), ukiziba masikio ya hizi noise na kujaribu kutafuta signal, utaona kuna kisasi fulani kinafanywa. Machawa wengi wanapumbazwa wasijue hata wao mwishoni watamalizwa.

Nchi imeshakuwa distabilized, chuki imejengeka, ile Tanzania ya udugu haipo tena, vultures walioitamani nchi yetu kwa miaka mingi wameshanusa harufu ya mizoga.
 
Hakuna cha watu wa nje wala nini? wauaji ni haohao police waliopewa hiyo kazi, hii ni kutaka kupoteza ushahidi muda ukifika, police na Samia mtalipa tuu haya mauaji ya watanzania wanaodai haki zao
 

Hii ni hatari sana hususan kwa Mkenya yeyote kuwa Tanzania kipindi kama hiki, utachukiliwa na kulazimishwa ukiri chochote.
 
Sawa
Sawa,
Vipi wale raia ambao ni bodaboda halali lakini kwa polisi kuwahisi kua ndio hao wasio raia wakaishia kuwaua pasipo hata kuwauliza au kuwakagua??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…