GE2025 Day 5: Polisi wasema kuna wageni wameingia nchini kuchochea vurugu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
ICC , CASE FILED HARAKA SANA ,NA WAHUSIKA WAKAMATWE HARAKA SANA, HII HAIKUBALIKI
 
You can fool some people some time....

Wageni wamekuwa wengi mpaka kulishinda jeshi la Polisi 🤔🤔🤔. Nchi ina usalama gani sasa?
 
Maskini bodaboda wa watu wameingiliwa, kazi yao itakua ngumu sana kipindi cha hivi karibuni.

Pole in advance bodaboda, zigo la nnya this time limewaangukia ninyi.
 
Umenikumbusha enzi za kamanda Suleiman Kova aliyemkamata mkenya kanisani kwa "Gwajima"? kufanya toba baada ya kumteka Dr Ulimboka .
 
Watu wanaingia nchini na kusambaa kote huko hatukujua??!!! Walikua wangapi??? Tusiposhugulikia shida zetu na kuanza kukwepa mm naona sio sahihi.
 
Kwamba watu wengi kiasi hicho sio watanzania.
Je, wameingiaje kama mnajidai kuwa mna intelijensia kubwa?
Ifikie mahali watu waliofaulu kwa division 1 ndio wakasomee upolisi.
 
Jeshi linalinda mipaka ina maana hao watu walipitia njia gani ili jeshi lisiwagundue ikiwa kwenye maji jeshi lipo na ardhini jeshi lipo na bila shaka airports jeshi lipo?

Silaha walipewa na nani za kuja kushambulia raia maana nina hakika hawakuingia na hizo silaha mipakani?
 
Ukweli utafahamika tu, ni suala la muda.🙏
 
Kama hao mliowaua si raia wetu, basi mrudishe maiti nchini mwao. Haya ni yale mambo yaliyotokea wakati Mwigulu Nchema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani, kulikuwa na mauaji ya watanzania wengi wakawekwa kwenye mifuko ya Sandarusi. Mwigulu akasema ni wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wanaoenda South Africa. Mbona hamkuwarudisha kwao ETHIOPIA kama ni kweli? Tatizo la polisi wetu na rais wao ni form IV failures hawajui wanachoongea, uwezo wao wa kufikiri umegota hapo.
 
Wakati hao watu wengi hivyo wanaingia nyie mlikua wapi? Mpaka raia ndio wawape taarifa?Acheni mambo yenu wazee
 
Dah kumbe Tanzania ina wahamiaji haramu wengi mno! Heads must roll ya wahusika na usalama wa nchi pamoja na uhamiaji kama haya yanayosemwa ni kweli, akiwemo huyu msemaji hapa kwani nae anahusika na ulinzi wa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…