Dayna:diamond kaniibia wimbo wa 'my no.1'

Dayna:diamond kaniibia wimbo wa 'my no.1'

mbeyatz

Senior Member
Joined
Jul 2, 2013
Posts
150
Reaction score
32
Kufuatia kutoka kwa hit ambayo inapewa sapoti na video ya mapesa mengi, My Number One ya Diamond Platinumz, Mambo yameanza kuwa mambo baada ya msanii Dyna Nyange kuibuka na kudai kuwa mdundo wa ngoma hii ulikuwa ni wa kwake na ulikuwa ni kwaajili ya wimbo ambao ulikuwa aufanye akiwa amemshirikisha msanii huyo.

Bado tunacheki mishe za kumpata Diamond kwaajili ya kulizungumzia swala hili kwaajili ya kupata uhalisia wake katika mdundo huo ambao unapewa credit kuwa umetengenezwa na Sheddy Clever.

Baada ya kupata story kuhusiana na mchongo huu, tukaamua kumvutia waya producer Sheddy Clever ambaye amesema kuwa kwa sasa hivi hayupo tayari kulizungumzia swala hili.

Dyna leo hii amenitumia ngoma hii anayolalamika kuwa amefanyika 'chimpupute' na Diamond Platinums so in sam few minutes, nitaiweka uweze kuisikiliza na kutoa maoni yako.

source: SAMMISAGO.blogspot.com
 
Hilo NASIBUDOMO ni jizi sana la nyimbo za wasanii wenzake na hii si mara ya kwanza kufanya hivyo kwani lilishawahi kumuibia wimbo H BABA na kuufanya wake.
 
Mbona hues hawatoi Brio Mutu akitoa tujue kaiba.mnauza wenyewe kwa shading ya kupata promo.scheming upuuzi. NA leaning hamjui ilipo cosota ukisha maliza kutunga Kazi Yakobo nenda kaisajili
 
Nilikuwa namuonea huruma dyna ila amenishangaza kwa haya:
1. Kumbe alisikia wimbo wa diamond kabla ya kuachiwa hewani na akasikia beat lake limetumiwa hakuchukua hatua wala hakumuuliza diamond wala shedy clever wala kusema kwenye media mpaka alipoona mwenzake kaachia huu wimbo? Kwanini hakusema mapema. Yeye ndiye kachemka.
2. Anasema hakusema kwakuwa alikuwa hajui nini afanye sasa ina maana ashapata solution au?

Inawezekana kweli kaibiwa lakini kitendo cha kujua kuwa ameibiwa akakaa kimya aje kupiga kelele sasa kwangu naona ni ujinga
 
Mkuu inawezekana walielewana nini sasa baada ya kuona jamaa kaurusha ndo anajitokeza
 
Inasemekana alikubaliana bei ya hyo beat na sheby clever lakn yeye akadelay kutoa mkwanja diamond akaenda kulichukua.so me naona diamond hana kosa na isitoshe hata lyrics alikua hajaingiza kweny beat wala hajainunua so amlaumu sheby clever.je angei2mia hyo beat angeitendea hak kama diamond?
 
Back
Top Bottom