Wanaojua jambo hawana sababu ya kuweka figisu figisu; wataongea uhalisia bila kupinda maneno! Sio siri, nilipokuwa nasikiliza ile clip ya D'Banj sikutarajia kama mwanamuziki mkubwa kama yeye angejishusha kiasi kile na kuelezea wazi wazi ni namna gani bado anahitaji collabo na Diamond!!!
Nakumbuka mwaka jana Chibu alipokuwa South Africa na kutangaza msululu wa wasanii wanaoimba collabo na yeye, kama kawaida yao; watu wakasema anatafuta kick lakini few months later ikaja kudhihirika baada ya ngoma moja baada ya nyingine kuanza kudondoka!