Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Awali ikumbukwe Mdau alieleza “Mkataba wa TARURA - Katavi waliosaini Novemba, 2024 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na Daraja la Milala Shongo walisema una gharama ya Tsh. Milioni 500 na kwamba ujenzi utakamilika Juni 2025, lakini mpaka sasa (Agosti 2025) hakuna jipya.”
Kusoma hoja yas Mdua bonyeza hapa ~ TARURA Katavi nauliza mkataba wa Tsh. Mil 500 na mkandarasi ulishia kuchimbua barabara na daraja?
Hali ilivyokuwa awali.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi, Jamila Yusuph amefika eneo la tukio na kueleza kuwa ujenzi ulisimama kutokana na mvua lakini watahakikisha Mradi unakamilika kwa kuwa wanafahamu umuhimu wa mradi huo.
Upande wa Hoza Joseph ambaye ni Meneja TARURA MPANDA amesema Mkandarasi amesharejea site na anaendelea na shughuli, mara ya kwanza waliweka zege kubwa yenye nondo na imekamilika, kinachofanyika kwa sasa Mkandarasi anavunja mawe na kuyasogeza eneo husika.