DC afika eneo la Mtemi Beda, asema ujenzi wa Barabara na Daraja ulikwama sababu ya mvua, Mkandarasi amerejea ‘site’

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Your browser is not able to display this video.
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia eneo la Mtemi Beda, Wilaya ya Mpanda akieleza limekuwa kero kero ya muda mrefu kutokana na changamoto ya ubovu wa Barabara ya Mtaa wa Misukumilo kwenda Kitongoji cha Milala Shongo Kijiji cha Milala, ufafanuzi umetolewa sababu ya kukwama kwa mradi huo.

Awali ikumbukwe Mdau alieleza “Mkataba wa TARURA - Katavi waliosaini Novemba, 2024 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na Daraja la Milala Shongo walisema una gharama ya Tsh. Milioni 500 na kwamba ujenzi utakamilika Juni 2025, lakini mpaka sasa (Agosti 2025) hakuna jipya.”

Kusoma hoja yas Mdua bonyeza hapa ~ TARURA Katavi nauliza mkataba wa Tsh. Mil 500 na mkandarasi ulishia kuchimbua barabara na daraja?

Hali ilivyokuwa awali.​

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi, Jamila Yusuph amefika eneo la tukio na kueleza kuwa ujenzi ulisimama kutokana na mvua lakini watahakikisha Mradi unakamilika kwa kuwa wanafahamu umuhimu wa mradi huo.

Upande wa Hoza Joseph ambaye ni Meneja TARURA MPANDA amesema Mkandarasi amesharejea site na anaendelea na shughuli, mara ya kwanza waliweka zege kubwa yenye nondo na imekamilika, kinachofanyika kwa sasa Mkandarasi anavunja mawe na kuyasogeza eneo husika.
 

Nchi yetu inachezewa sana,

Lakini yana mwisho, ni suala la muda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…