Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Serikali imezungumzia suala la madai ya Wananchi wa Kijiji cha Imalamate katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu kulalamikia changamoto ya Mgodi wa Dhahabu wa EMJ kwamba unamwaga maji yanayodaiwa kuwa na sumu kwenye mto.
Mgodi huo ambao unamilikiwa na Mzawa pamoja na raia wa kigeni unadaiwa kusababisha athari kwa Wananchi kutokana na hali hiyo ya maji hayo kumwagika kwenye mto ambao ni chanzo cha maji kinachotumiwa na Wananchi wengi.
Zaidi kuhusu hoja hiyo ~ Simiyu: Serikali itusaidie, Mgodi wa Dhahabu EMJ unatiririsha maji yanayodaiwa kuwa na ‘sumu’ katika mto
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Faiza Salim amezungumza na JamiiFourums na kufafanua:
Hilo lilikuwa tukio la maji kupenya nje ya mgodi ilitokea Mwaka jana (2024), ni takribani miezi nane iliyopita.
Kilichotokea sehemu ya kuhifadhia maji ilipasuka kutoka katika mgodi, tukaita watu wa NEMC kutokana na kadhia hiyo, taratibu zilifanyika wahusika wa mgodi wakapewa adhabu na huduma zikasitishwa hadi watakapotimiza maelekezo waliyopewa.
Waliweza kukamilisha taratibu zote zilizotakiwa, inawezekana huyo aliyeandika alimaanisha tukio la zamani, hiyo kesi mpya haijatufikia.
Wahusika walikamilisha taratibu zote walizopewa na watu wa mazingira, wakapewa certificate wakaendelea na shughuli zao, sijapokea changamoto mpya kuhusu suala hilo kama ipo.