DC Chongolo: Wanaowatembeza walemavu mitaani wanaweza kushtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh Chongolo amesema wale wote waliokamatwa katika zoezi la kukamata wanaowatumikisha walemavu wametenda kosa la jinai.

Chongolo amesema wahusika wa miradi hii watashtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu.

Walemavu waliokamatwa wengi wanatoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita na wachache wametokea Kigoma na Kagera.

Kwa sasa uchunguzi unaendelea ukihusisha wizara ya Tamisemi, Mambo ya ndani, Katiba na Sheria pamoja na ofisi ya Waziri mkuu.

Mahojiano yako mubashara Channel ten yakimuhusisha pia Naibu waziri Ummy anayeshughulikia walemavu.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
 
Kusafirisha binadamu sio kosa, kosa ni kusafirisha binadamu kinyume na sheria/taratibu kwenye baiskeli yenye magurudumu 2/3.

Mfano; Gari, bajaji, pikipiki zina taratibu ila hizo zingine za magurudumu hazina utaratibu huo tajwa, ispokua kama zinatumika kwa muhusika kwa kusudi kusudiwa.
 
Mfano; Gari, bajaji, pikipiki zina taratibu ila hizo zingine za magurudumu hazina utaratibu huo tajwa, ispokua kama zinatumika kwa muhusika kwa kusudi kusudiwa
DC ameeleweka!
 
Utakuta jitu mbavumbavu kutwa linazurura na mlemavu kwenye mabaa kama ni ndugu yake si amuache nyumbane afanye kazi akamuhudumie?? aisee wasakwe wakamatwe naunga mkono hoja
 
Hii tabia hata mimi nimeichoka, hao walemavu miaka yote wanatembezwa tu hawapati mitaji wafanye biashara? au wameshageuza kuomba omba ndio biashara yao, haina kuwekeza mtaji, ni faida tu kila siku.

Wamekuwa too much, ukiwa kwenye gari wanagonga dirishani, ukienda bar wapo, barabarani ukitembea wapo, sasa kwa siku tuwasaidie wangapi? au ndio tuanze kutembea na "budget" ya walemavu, usawa unakaba jama.
 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh Chongolo amesema wale wote waliokamatwa katika zoezi la kukamata wanaowatumikisha walemavu wametenda kosa la jinai.

Chongolo amesema wahusika wa miradi hii watashtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu.

Walemavu waliokamatwa wengi wanatoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita na wachache wametokea Kigoma na Kagera.

Kwa sasa uchunguzi unaendelea ukihusisha wizara ya Tamisemi, Mambo ya ndani, Katiba na Sheria pamoja na ofisi ya Waziri mkuu.

Mahojiano yako mubashara Channel ten yakimuhusisha pia Naibu waziri Ummy anayeshughulikia walemavu.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!

Bwahaaa bwahaaaa, nimecheka kwa nguvu kinoma. Kweli Magu ametuharibia nchi kwa kupandandikiza siasa za kiki. Sasa kiki zinabackfire viongozi wanageuka futuhi.
 
Hii tabia hata mimi nimeichoka, hao walemavu miaka yote wanatembezwa tu hawapati mitaji wafanye biashara? au wameshageuza kuomba omba ndio biashara yao, haina kuwekeza mtaji, ni faida tu kila siku.

Wamekuwa too much, ukiwa kwenye gari wanagonga dirishani, ukienda bar wapo, barabarani ukitembea wapo, sasa kwa siku tuwasaidie wangapi? au ndio tuanze kutembea na "budget" ya walemavu, usawa unakaba jama.
Sio kosa kuwa omba omba!
 
Kusafirisha binadamu sio kosa, kosa ni kusafirisha binadamu kinyume na sheria/taratibu kwenye baiskeli yenye magurudumu 2/3.

Mfano; Gari, bajaji, pikipiki zina taratibu ila hizo zingine za magurudumu hazina utaratibu huo tajwa, ispokua kama zinatumika kwa muhusika kwa kusudi kusudiwa.

Hapo kusafirisha binadamu ni 'human trafficking' iliyotoholewa, kosa liko pale pale.

Sio kuwasukuma, bali ni ile kuwakusanya kutoka mikoani na kuwasafirisha... kwa lengo la kuja kuwachuuza mjini.
 
Utakuta jitu mbavumbavu kutwa linazurura na mlemavu kwenye mabaa kama ni ndugu yake si amuache nyumbane afanye kazi akamuhudumie?? aisee wasakwe wakamatwe naunga mkono hoja
Kuna kisa kimoja nilikiona nikasema sitakuja kumpa hela ombaomba. Nitatoa msaada hospitali, jela na vituo vya yatima na wazee
 
Back
Top Bottom