DC Chongolo: Wanaowatembeza walemavu mitaani wanaweza kushtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu!

DC Chongolo: Wanaowatembeza walemavu mitaani wanaweza kushtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu!

Kwa uhuni nilioushuhudia pale udsm miaka hiyo, nikasema katu sitakuja kutoa hela yangu kwa hawa omba omba..
 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh Chongolo amesema wale wote waliokamatwa katika zoezi la kukamata wanaowatumikisha walemavu wametenda kosa la jinai.

Chongolo amesema wahusika wa miradi hii watashtakiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu.

Walemavu waliokamatwa wengi wanatoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita na wachache wametokea Kigoma na Kagera.

Kwa sasa uchunguzi unaendelea ukihusisha wizara ya Tamisemi, Mambo ya ndani, Katiba na Sheria pamoja na ofisi ya Waziri mkuu.

Mahojiano yako mubashara Channel ten yakimuhusisha pia Naibu waziri Ummy anayeshughulikia walemavu.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
So sad.

Naona safari hii Dodoma imepata hati safi
 
Back
Top Bottom