DC Hashim Komba: waliouziwa ardhi kuanzia mwezi Juni 2020 mpaka Disemba 2021, rudisha Ardhi hiyo kwani ni batili

DC Hashim Komba: waliouziwa ardhi kuanzia mwezi Juni 2020 mpaka Disemba 2021, rudisha Ardhi hiyo kwani ni batili

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wananchi wilayani Nachingwea mkoani Lindi waliouziwa ardhi katika vijiji mbalimbali kuanzia mwezi Juni 2020 mpaka Disemba 2021 wametakiwa kurudisha Ardhi hiyo kwani mauziano hayo ni batili.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Hashim Komba alipokuwa akizungumza katika mkutano maalumu wa uzinduzi wa muongozo wa umilikishaji ardhi ambapo ameeleza kuwa, serikali ilisitisha ugawaji wa ardhi tangu mwaka 2020 mwezi wa 6 mpaka pale watakapotoa muongozo rasmi, lakini licha ya katazo hilo bado watu walikubali kuuziwa ardhi, hivyo warudishe na mauziano hayo ni batili.

Chanzo: Radio Mashujaa
 
Mh ameanza kulewa madaraka? Si bure nyuma yake kunakivuli kinamsemesha
 
1640819503589.png
 
UFAFANUZI KUHUSU HOJA YA ARDHI ZA VIJIJI ZILIZOUZWA KIHOLELA NACHINGWEA

By Hashim Komba (DC Nachingwea)

Salaam,
Awali ya yote niseme Habari zinapoandikwa kwa ufupi bila kutoa maelezo ya kina huleta Taharuki isiyo na msingi

Utangulizi:
-Kwa muda mrefu sasa wilayani kwetu kumekua na migogoro ya Ardhi mingi inayosababishwa na mauziano holela yanayofanywa na baadhi ya viongozi wa vijiji wasio waaminifu na bila kushirikisha mikutano ya vijiji kama utaratibu unavyotaka.

Hali hii imepelekea athari zifuatazo
1.Hifadhi za misitu ya vijiji kuuzwa KIHOLELA
2.Kutozingatiwa kwa mipango ya matumizi bora ya Ardhi(ambapo wafugaji kuwekwa maeneo ya kilimo na wakulima kuwekwa maeneo ya mifugo,,hii hupelekea migogoro ya wakulima na wafugaji.
3.Upotevu wa mapato ya serikali za vijiji.
4.Wananchi kuuziwa Ardhi moja kwa mtu zaidi ya mmoja.
5.Wananchi kutojumuishwa ktk kufanya Maamuzi ya Ugawaji wa Ardhi za vijiji vyao.

Baada ya Athari hizo kujitokeza tulikubaliana sasa kuwa ni vyema Wataalamu wa Ardhi wakapitia sheria za Ardhi ,sera ya ardhi ili kutoa mwongozo utakaotumika kuwaongoza vyema vijijini ili kusaidia kumaliza migogoro ya Ardhi inayoendelea.

Aidha,tayari Mwongozo huo umekamilika ambao umeandaliwa na kupitiwa na Kamishna wa Ardhi ngazi ya Mkoa.

Ktk Kipindi cha Mpito Kuna baadhi ya viongozi wa vijiji waliendelea kuvunja sheria ikiwemo Kugawa Ardhi zaidi ya hekari 50.Kugawa hekari 100/200/300 na kuendelea wakati sheria inawapa mamlaka ya ugawaji Ardhi mwisho hekari 50.

-Maeneo mengine mikutano ya vijiji haikufanyika lkn watu wachache wakafanya ugawaji Ardhi kwa watu na kuleta malalamiko kwa Wananchi

-Maeneo mengine Kuna wenyeviti wa vijiji wamediriki kupokea fedha na kuweka mifukoni mwao bila kupitisha maamuzi hayo ktk serikali za vijiji wala kutumia Akaunti za vijiji

KIPI KILICHOELEKEZWA KUHUSU KUREJESHA ARDHI;;

1.Agizo limewataka wote waliouziwa Ardhi hizo kinyume na Taratibu kujitokeza ktk Serikali za Vijiji ili wajiorodheshe huko na kueleza ni utaratibu upi waliutumia kupata Ardhi husika ili waisaidie serikali ktk Kubaini ubadhirifu uliofanywa na wasiozingatia taratibu pamoja na miongozo ya serikali.

2. Agizo limewataka baada ya Kujikabidhisha ktk serikali za vijiji, Watapewa utaratibu wa namna ya Kuiomba hiyo Ardhi ili waweze kumilikishwa upya kwa kuzingatia Miongozo iliyopo pamoja na kudhibiti upotevu wa maduhuli ya serikali

NB:
-Kupitia zoezi hili wale wote ambao itabainika walidhulumiwa fedha zao kwa kulipa fedha nyingi zaidi kinyume na utaratibu,viongozi waliohusika watawajibika kulipa fedha hizo kumrejeshea mnunuzi wa Ardhi.

-Kupitia Agizo hili fedha zote za kumilikishwa Ardhi ambazo ziliishia mifukoni mwa watu sasa zitaingia ktk Akaunti za Vijiji.

-Kupitia Agizo hili sasa Ardhi itagawiwa upya kwa kuzingatia dhana ya Ushirikishaji wa Wananchi ili Mikutano ya Vijiji ihusike Kugawa Ardhi kama inavyotakiwa na Sheria.

-Kupitia Agizo hili sasa wawekezaji wetu waliokuwa wanatozwa fedha zilizo nje ya utaratibu kwa manufaa ya watu binafsi watakwenda kusaidiwa wasidhulumiwe haki zao na wajanja wachache.

Mwisho:
-Nitoe Rai kwa Wadau wa Habari kuchanganua vyema Habari wanazoandika ili kutoleta mkanganyiko kwa Jamii au kutoa Habari inayozalisha maswali mengi bila majibu.

Wajibu wetu ni kuhakikisha tunapambana kuipunguza migogoro ya Ardhi kama si kuimaliza ndani ya wilaya yetu.

Hashim .A.Komba
DC NACHINGWEA
Wananchi wilayani Nachingwea mkoani Lindi waliouziwa ardhi katika vijiji mbalimbali kuanzia mwezi Juni 2020 mpaka Disemba 2021 wametakiwa kurudisha Ardhi hiyo kwani mauziano hayo ni batili.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Hashim Komba alipokuwa akizungumza katika mkutano maalumu wa uzinduzi wa muongozo wa umilikishaji ardhi ambapo ameeleza kuwa, serikali ilisitisha ugawaji wa ardhi tangu mwaka 2020 mwezi wa 6 mpaka pale watakapotoa muongozo rasmi, lakini licha ya katazo hilo bado watu walikubali kuuziwa ardhi, hivyo warudishe na mauziano hayo ni batili.

Chanzo: Radio Mashujaa
 
Back
Top Bottom