Elections 2010 DC Igunga ni mkristo mkatoliki; Kwanini hajasema kitu?

Kwa hiyo ile hoja kuwa BAKWATA ni kitengo cha propaganda cha CCM imepata ushahidi. Ila sikubaliani na baadhi ya wana JF kushusha lawama na kejeli kwa Waislamu.Uwakala wa CCM unafanywa na viongo wachache wa BAKWATA wakiongozwa na njaa zao, ni jukumu la Waislamu wenyewe kuwapinga hadharani mashehe wao walionunuliwa na mafisadi wa CCM.Natoa mwito kwa wana jamvi hapa JF kuacha mara moja kushusha lawama kwa Waislamu na Uislamu kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaingia mtego wa CCM wa kutugawa kwa misingi ya dini ili wao waendelee kutufukarisha. Na kama tuna kumbu kumbu nzuri, kwa miaka mingi BAKWATA imekuwa ikilalamikiwa na Waislamu wengi tu kuwa hai tetei maslahi yao lakini BAKWATA imeendelea kudumu kwa kukingiwa kifua na serikali ya CCM hivyo wanachofanya BAKWATA ni kulipa fadhila kwa CCM.
 
"Msiipigie kura chadema, wamemzalilisha mwanamke wa Kiislamu"
Hivi huyu aliyetoa wito huu anajiskiaje sasa hivi akigundua kumbe DC sio Mwislamu. Da!!
 
 
"Msiipigie kura chadema, wamemzalilisha mwanamke wa Kiislamu"
Hivi huyu aliyetoa wito huu anajiskiaje sasa hivi akigundua kumbe DC sio Mwislamu. Da!!

mkuu, hajisikii lolote, si unajua kila mwendawazimu ana fani yake (alfuunun majuunun)
 
well said bro..
 
Hili swali linatakiwa kujibiwa na viongozi wa Bakwata tena wao waiombe Chadema msamaha!
 
Mimi ni mkristo mkataliki, lakini bado siwezi kuwajumlisha waislamu wote kwenye upuzi huo wa Bakwata kutumiwa na CCM. Isipokuwa nawakumbusha waislamu kuwa msikubali kuyumbishwa na Bakwata ambao ni vizabizabina wa CCM na lecca culo wakubwa na ccm na serikali yake. Walichofanya Bakwata ni aibu kubwa sana, kumtetea Dc mkatoliki na kuishutumu Chadema.Sasa tunawataka watuambie sisi wana wa Igunga kuwa kura zetu bado tuziwape Chadema? je tuwape hawa wahuni CCM wabaoifanya Bakwata idharaulike namna hii kwa kauli zao za kuganga njaa na wala sio kwa misingi ya dini.Kwa hilo Bakwata wametia aibu, Aibu, aibu, aibu!
 
2nahtaji ushahidi wa cheti,jina la ubatizo.pia kuwa na mume mkatoliki haimaanish mke naye ni mkristo mkatoliki.huwenda wanaish km bibi na bwn kila mmoja akiwa na dini yake.
 

nimependa sana comment zako, hakika wewe ni mwislam unayejua uislam ni nini na una uchungu na uongozi wa bakwata.kweli kuna haja ya kuweka viongozi wenye elimu zote si elimu ya dini tu kwani mambo mengine yanayohitaji maamuz siyo yote yanayohusu iman au din bali yanahitaji skills nyingine.
 
mkuu! hii habari nikweli? mama yangu! sasa hawa bakwata watajificha wapi? nahuyu mama sindokajishushia heshima kabisa hadi kwa ndugu zake jamani!

mama fatuma kimario umeshusha hadhi yakinamama!

nanyie bakwata acheni kutumika!
Haya ndo matatizo ya hawa ndugu zetu; kazi yao ni kukurupuka na kukubali kutumiwa na CCM kila mara. Hawajifunzi tu? Marangapi wamedanganywa na CCM. Kazi kwelikweli
 
Kama ni hivyo mama amejishushia hadhi kabisa mbele ya jamii inayomzunguka, kwanini asingetoka hadharani asema yeye si muislam, au ameambiwa asitoe siri kuwa alisha batizwa.
Analinda kibarua chake huyo,hawezi sema.
 


Purely nonsense brains, takribani ni miaka zaidi ya elfu tangu kuzaliwa kwa uislamu hivi kweli hamjawahi kuelimishwa na kuifahamu hijabu ni kitu gani mpaka Maa-Shura ya Maimam au Bakwata wawaambie kuwa hii sasa ni hijabu. Yaani mwanaume au mwanamke hawezi kujua kwamba sasa nimevaa hijabu au la!! Mbona mnaongea mambo ya kuzidi kujidhalilisha kihivyo. Kwa hiyo wanawake wa kiislamu ili kujihakikisha kuwa wamevaa hijabu au la huwa kwanza wanaenda kwa shura ya Maimamu na bakwata kuthibitisha kwamba kweli walivyovaa ni hijabu. Yaani mwislamu hawezi kujua kwamba alichovaa mke wake ni hijabu au sio hijabu. Du!! Hii kali imenitoa na povu bila kujua. Basi kama ni hivi na mawazo ya hivi, akili za hivi, kweli watanzania tunayo safari ya kwenda. Poleni Watanzania wenzangu lakini tutafika hivyo kwa kujikongoja kidogo kidogo.
 
Reactions: Nzi

Kwa hiyo hapo kwenye red miaka elfu na zaidi Waislamu hamjui ku-define hijabu mpaka shura ya maimamu na Bakwata waseme hii ndo hijabu. Du! Kazi mnayo kweli, kama hilo tu ni tabu kulifahamu lipi sasa mtalijua na kukua kiimani. Maana nafikiri hilo ni miongoni ya mafundisho ya msingi kabisa na nyie bado hamjui, haya na hadithi za mtume zitaeleweka kweli???
 
Reactions: Nzi
chokochoko za kidini na muungano ndiyo vitu viwili vinavyonifanya wakati mwingine nijutie kuwa Mtanzania. Kwa bahati mbaya sina kwingine ninakoweza kupaita nchi yangu.
 

Nje ya mada.
 
sijui MSAHAFU unasemaje kuhusu hilo, mie nasimamia DINI MOJA YA KRISTO, wengine wanaiita UKRISTO. Kwa mjibu wa BIBLIA, hakuna madhehebu, wala hayajatamkwa mahala popote pale. Ndicho ninachokijua

Anzisha thread mpya kwa mjadala huo wa dini.
 
Tatizo naloliona hapa ni pale wakristu wanapojaribu kutafslri Uislaam hali hawaujui hata kidogo..Hijab ni vazi la mwanamke awe Muislaam, Mkristu au Budha haijalishi kwa sababu dini inasimamia haki za wanawake wote.

Tatizo la Bakwata ktk madai yao yaliyozungumzia mwanamke wa kiislaam kuvuliwa Hijab na haikuwa swala la mwanamke yeyote kwa sababu Tanzania yetu Uislaam ni jina na uzawa wa mtu, na ndivyo siku zote masheikh Mapadre na wananchi wote wamekuwa wakitafsiri dini zetu kwa uzawa na Ubatizo na sii ibada zake.

Tafisri kamili ya Hijab ni mtandio, kilemba au vazi lolote zinalofunika nywele za mwanamke...Hizi habari za Hijab lazima iwe ya Kiarabu au kiOman ni utumwa wa akili ulotokana na Ulimbukeni kwa sababu hata mama zetu wanaovaa khanga kichwani huvaa hijab vile vile.. Ni ujinga mkubwa sana kuendelea kutumia maneno ya kiarabu na tukashindwa kuyatafsiri kulingana na mazingira yetu.

Na hakika Bakwata wamefanya makosa kuzungumzia Uislaam wa Hijab kwa mtu ambaye hafuati hata ibada mojawapo ya kiislaam kueteta mwanamke ambaye sii tu alivuliwa mtandio bali pia viatu na mkufu pengine wenye msalaba... Hivyo, kama swala ni haki ya wanawake kukanya udhalilishaji wa wanawake tayari vyombo vyetu vya sheria vimeshapokea mashtaka na kesi ipo mahakamani..

Bakwata ni chombo cha CCM na kitaendelea ku tetea maslahi ya CCM kwa kuitumia dini na chombo hiki ni hatari zaidi ya chama CCM chenyewe. Maneno haya niliwahi kuambiwa na Sheikh Kassim bin Jumaa katika uhai wake na toka siku ile sikuwa na imani na chombo hiki. Wapo marafiki zangu waliojaribu sana kupingana na Bakwata, mwisho wake walikuwa wao magaidi na walitafutwa na vyombo vya usalama ya kuwa wao ni hatari kwa usalama wa nchi..Na wengine wamepoteza maisha yao!..
 

Gaijin,

Huwa sipendi kuongelea threads zenye mambo ya kidini lakini naona kwa hili wanasiasa wanataka kutuchonganisha kwa kutumia dini zetu kwa manufaa yao binafsi. Baada ya kusoma bandiko lako ilinibidi nikasome tamko la BAKWATA. Aya ya tatu ya tamko inasema
"kitendo cha unyanyasaji, udhalilishaji na dharau ya hali ya juu kwa wanasiasa wa CHADEMA kumvua hijabu mama wa Kiislamu - DC wa Wilaya ya Igunda." Aya ya tano yenye tamko lenyewe inasema "Watuhumiwa wamemdhalilisha mama wa Kiislamu Bi. Fatuma Kimario...." Sikiliza tamko kwenye video hapo chini; ambapo emphasis inaonekana zaidi kwenye "mama wa Kiislamu."

Sio kwa kwamba ninawatetea watuhumiwa simply because siwezi kuwatetea. After all kesi tayari iko mahakamani. Lakini malalamiko ya BAKWATA yanaonyesha sio juu ya mwanamke kudhalilishwa bali mwanamke wa Kiislamu kudhalilishwa. I just wish wangekuwa general kama ulivyoandika au Bi Fatuma angetoa statement na kusema yeye ni Muislamu. Had BAKWATA not been specific kuwa aliyeladhilishwa ni mwanamke wa Kiislamu wala tunsingekuwa tunajadili haya. Kama kinachosemwa ni kweli, kulingana na statement ya BAKWATA inaoneyesha kama vile walikuwa hawajui background ya huyu mama.

Hata hivyo, kitu ambacho naona kimesahaulika kabisa kujadiliwa ni kuhusu hivi vyombo vinavyotetea wanawake. So far sijasikia hata chombo kimoja kikitoa statement kuhusiana na yaliyomkumba huyu mama. Badala yake suala limekuwa ni la kidini zaidi. Dini, kamwe haiwezi kuwa ni chanzo cha kinzani, chuki na uhasama kati ya watu. Baadhi ya wanasiasa wanatumia dini kwa ajili ya mafao yao binafsi kwa kukazia kinzani.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…