SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Kwa hiyo ile hoja kuwa BAKWATA ni kitengo cha propaganda cha CCM imepata ushahidi. Ila sikubaliani na baadhi ya wana JF kushusha lawama na kejeli kwa Waislamu.Uwakala wa CCM unafanywa na viongo wachache wa BAKWATA wakiongozwa na njaa zao, ni jukumu la Waislamu wenyewe kuwapinga hadharani mashehe wao walionunuliwa na mafisadi wa CCM.Natoa mwito kwa wana jamvi hapa JF kuacha mara moja kushusha lawama kwa Waislamu na Uislamu kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaingia mtego wa CCM wa kutugawa kwa misingi ya dini ili wao waendelee kutufukarisha. Na kama tuna kumbu kumbu nzuri, kwa miaka mingi BAKWATA imekuwa ikilalamikiwa na Waislamu wengi tu kuwa hai tetei maslahi yao lakini BAKWATA imeendelea kudumu kwa kukingiwa kifua na serikali ya CCM hivyo wanachofanya BAKWATA ni kulipa fadhila kwa CCM.