kwa mujibu wa Gazeti la Mwanahalisi la leo tar 28 Septemba hado 04 Oktoba DC Fatuma Kimario anyedaiwa kuvuliwa Hijabu, sio muislamu. Ameolewa na Mtu wa dhebu la Kikristo na amezaa naye watoo wanne. Mtoto mmoja aitaye Vivian (Mkristo) anatarajiwa kufungqa ndoa ya kikatoliki mwezi Oktoba 2011. Alipohojiwa Ustaadh Amir Said Amir kuhusu suala hilo alinukuliwa akisema kuwa "watu wengi hudhani kuwa Uislamu ni jina. Uislamu ni imani na matendo mema. Kila mtu anaweza kujiita muislamu lakini kama hafuati misingi, hata kama amevaa hijabu, siyo muislamu.
Sheria ya Kiislamu inaema ndoa ya kiislamu itafungwa kwa kuzingatia muongozo wa kurani na maelekezo ya Mtume Muhammad (SAW). Kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya Kuraani (suatul Mumtahinnah aya ya 10), mwanamke wa kiislamu amabye ameolewa na na asiyekuwa muislamu, basiametoka katika dini hiyo (muttaddah).
Naye meanazuoni mashuhuri nchini, Sheikh Issa Ponda alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema "Kwanza hakuna ndoa kati ya muislamu na asiyekuwa muislamu, Mtu akifanya hivyo atahesabika anafanya zinaa." Kuhusu kubadili dini , Sheikh Ponda amesema "Hilo ni kosa kubwa sana. Mtu wa aina hiyo, anakuwa ameleta mfano mbaya kwa uislamu. Anastahili kuadhibiwa kwa kupigwa mawe hadi kufa kutokana na kuritadi (kuondoka kwenye uislamu)"
NAOMBA KUWASILISHA. HONGERA SANA MWANAHALISI KWA UTAFITI WENU.