The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James ametoa siku 14 kwa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani humo kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kisheria kuzuia vitendo vya mara kwa mara vya uvamizi wa hifadhi za barabara vinavyosababishwa na ongezeko la shughuli za kibinadamu ikiwemo biashara ndogo ndogo na hivyo kusababisha kadhia kwa watumiaji wengine wa barabara.
Maagizo hayo yametolewa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) ambacho pia kimepokea taarifa mbalimbali za maendeleo ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya wilaya ya Iringa DC.