Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mkuu wa wilaya ya Iringa Komred Kheri James ameendelea kuwafikia Wananchi wa wilaya ya Iringa kupitia ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa, yenye lengo la kusikiliza Wananchi, kukagua miradi ya maendeleo, kuhamasisha shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma.
Akizungumza na Wananchi katika mitaa ya Kata ya Mkimbizi na Mtwivila, Komred Kheri James ameeleza umuhimu wa ushiriki wa Wananchi katika ajenda ya Usalama, Utunzaji wa Mazingira, Usafi, umuhimu wa Elimu,
na mapambano dhidi ya udumavu.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amewaomba watumishi wa Umma kuendelea kuwahudumia wananchi kwa wema na ukarimu ili kujenga misingi bora ya upatikanaji na utoaji wa huduma ili kujenga ustawi wa umma.
Katika ziara hiyo pia Wananchi wameendelea kupata fursa ya kushauri kuuliza na kutoa mtazamo wao juu ya mambo mbalimbali ambayo pia Serikali iliwapa ufafanuzi katika ziara hiyo.