DC Jerry Murro apiga marufuku mijadala ya Katiba

DC Jerry Murro apiga marufuku mijadala ya Katiba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
DC wa Ikungi Jerry Muro amepiga marufuku mijadala ya Katiba kwa wananchi wa wilaya hiyo pamoja na kusanyiko lolote linaloashiria kuhamasisha wananchi kujadili katiba pamoja na mikutano ya hadhara. DC huyo amesema wilaya hiyo haihitaji katiba bali inahitaji huduma kama maji, shule

Jerry-Muro.jpg
 
Kupiga marufuku Jambo linaaloruhusiwa na katiba huko ni kuivunja katiba.

Hata Rais mwenyewe hajakataza sijui Jerry Muro kapata wapi hiyo mamlaka.

Jerry tuambie umezuia kwa kutumia kifungu kipicha sheria tafadhali otherwise uondolewe kazini kwa kuvunja sheria
 
Katiba ya Nchi haifuatwi hata kidogo. Imekuwepo tu lakini yanayofanyika ni tofauti na yaliyomo katika katiba. Tanzania Tunahitaji Katiba mpya sasa.
 
Huu ndio udikteta wenyewe, uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kisheria kwa kila mtanzania, huyo Jerry asitake kuwafunga watu midomo.
 
Tuanze kuhesabu siku zake Jerry hii ni uchache wa elimu ya uraia
 
Kuna watu wanachanga karata vibaya sana ... huku katiba ... huku solidarity fund ...kule kodi ya nyumba na huyu naye kaanza kua Vasco da gamma wa kike mara mipasho ... kuna mtu au kikundi cha watu kina remote control
 
Kupiga marufuku Jambo linaaloruhusiwa na katiba huko ni kuivunja katiba.

Hata Rais mwenyewe hajakataza sijui Jerry Muro kapata wapi hiyo mamlaka.

Jerry tuambie umezuia kwa kutumia kifungu kipicha sheria tafadhali otherwise uondolewe kazini kwa kuvunja sheria
Hivi jamaa akili yake huwa iko sawa kweli ???!! Nadhan hii ndio type ya akina yule wa mkoa wa mwanza aliyetumbuliwa, nimesahau jina lake.
 
Jerry wacha Ujinga. Fanya kazi yako. Najua utasoma hapa. Nasema wacha UMAMA.
 
DC wa Ikungi Jerry Muro amepiga marufuku mijadala ya katiba kwa wananchi wa wilaya hiyo pamoja na kusanyiko lolote linaloashiria kuhamasisha wananchi kujadili katiba pamoja na mikutano ya hadhara.DC huyo amesema wilaya hiyo haihitaji katiba bali inahitaji huduma kama maji, shule
HUYO sio Mjinga, anasoma MOOD YA MAMA Bosy wake...KATIBA anaiita CHOKOCHOKO.

Hatakemewa, na kutakuwa na WAVE nchi nzima ya Matukio kupinga vuguvugu la katiba, kea lengo la "KUCHEZA NGOMA YA MAMA"
 
Back
Top Bottom