Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya hoja iliyotolewa na Mwanakijiji cha Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza kuwa kuna dampo kwenye makazi ya watu ambapo pia wanachoma taka na kuleta moshi unaosababisha Wananchi wavute hewa chafu usiku kucha, hatimaye hatua zimechukuliwa.
Mdau alidai Wananchi wanatozwa pesa kwa ajili ya uzoaji taka na wakaomba serikali ya Kijiji itafute eneo rafiki na si katika makazi ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi amesema hatua zimechukuliwa na kwamba Wakazi wa Kitongoji cha Usagara-A wamekubaliana na Mzabuni kuondolea taka zao kwenye Kaya kila Jumamosi.
Ameongeza kuwa wataendelea kutoa elimu ili eneo hilo lisitumike kama dampo tena.
Pia soma:
~ Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi tumewekewa dampo kwenye makazi ya watu
~ RC Mtanda: Suala la dampo katika makazi ya watu Kata ya Usagara, litashughulikiwa na DC na Halmashauri ya Misungwi