Baada ya hoja iliyotolewa na Mwanakijiji cha Usagara A, Kata ya Usagara, Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza kuwa kuna dampo kwenye makazi ya watu ambapo pia wanachoma taka na kuleta moshi unaosababisha Wananchi wavute hewa chafu usiku kucha, hatimaye hatua zimechukuliwa.
Mdau alidai Wananchi wanatozwa pesa kwa ajili ya uzoaji taka na wakaomba serikali ya Kijiji itafute eneo rafiki na si katika makazi ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi amesema hatua zimechukuliwa na kwamba Wakazi wa Kitongoji cha Usagara-A wamekubaliana na Mzabuni kuondolea taka zao kwenye Kaya kila Jumamosi.
Ameongeza kuwa wataendelea kutoa elimu ili eneo hilo lisitumike kama dampo tena.