DC Jokate: Hatulazimishi watu kufanya usafi, bali litakuwa zoezi shirikishi

DC Jokate: Hatulazimishi watu kufanya usafi, bali litakuwa zoezi shirikishi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
DC JOKATE: HATULAZIMISHI WATU KUFANYA USAFI, BALI LITAKUWA ZOEZI SHIRIKISHI

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo amezindua kampeni ya "Pendezesha,safisha Dar es salaam" yenye lengo la kusafisha mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza katika eneo la Zakhem Mbagala, ambapo kampeni hiyo imezinduliwa kiwilaya, Mhe. Jokate amesema hawatawalazimisha watu kufanya usafi,bali litakuwa zoezi shirikishi.

"Hii sio kampeni ya siku moja kama alivyoagiza Mhe.Mkuu wa Mkoa,tofauti kubwa ya sasa hatushurutishi watu kufanya usafi,bali tumetengeneza mazingira watu waone wajibu wao katika hili".Alisema Mkuu huyo wa wilaya

Ameendelea kusema kuwa suala la usafi linapaswa kuwa ni utamaduni wa kila Mwananchi, huku akionesha kufurahishwa na jinsi mazingira ya eneo la Mbagala yalivyo kwa sasa.

Uzinduzi huo wa kampeni ya usafi umehudhuriwa na mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Temeke Mhe.Abdallah Mtinika pamoja na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Ndugu Elihuruma Mabelya.

@jokatemwegelo

#safishapendezeshadaressalaam
#safishapendezeshatemeke
#kaziiendelee🇹🇿

IMG-20211204-WA0108.jpg


IMG-20211204-WA0112.jpg


IMG-20211204-WA0109.jpg


IMG-20211204-WA0110.jpg


IMG-20211204-WA0114.jpg
 
Back
Top Bottom