DC Julius Mtatiro: Nchi nyingi sana duniani hununua umeme kutoka Nchi Jirani kwa sababu mbalimbali

DC Julius Mtatiro: Nchi nyingi sana duniani hununua umeme kutoka Nchi Jirani kwa sababu mbalimbali

Nchi nyingi duniani hununua umeme kutoka nchi jirani kwa sababu mbalimbali, kama vile upungufu wa uzalishaji wa ndani, umbali wa umeme wa ndani unaopelekea umeme mwingi kupotea njiani, gharama nafuu ya umeme wa nje, na ushirikiano wa kanda. Hapa ni baadhi ya nchi zinazonunua umeme kutoka nchi nyingine:


AFRIKA

1. Tanzania – Inapanga kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia mpango wa Eastern Africa Power Pool (EAPP).
2. Kenya – Inanunua umeme kutoka Ethiopia na Uganda ili kuongeza upatikanaji wa nishati.
3. Rwanda – Inanunua umeme kutoka Uganda na Tanzania ili kufidia uhaba wa uzalishaji wa ndani.
4. Burundi – Inategemea umeme kutoka Rwanda na DRC.
5. South Africa – Inanunua umeme kutoka Msumbiji (Cahora Bassa Dam) na Namibia.
6. Botswana – Inanunua umeme kutoka Afrika Kusini kupitia Southern African Power Pool (SAPP).
7. Zambia – Inanunua umeme kutoka DRC na Afrika Kusini wakati wa uhaba.
8. Namibia – Inategemea ununuzi wa umeme kutoka Afrika Kusini na Zambia.

ULAYA

1. Uingereza – Inanunua umeme kutoka Ufaransa kupitia nyaya za chini ya bahari (interconnectors).
2. Ujerumani – Inanunua umeme kutoka Ufaransa na Denmark, hasa umeme wa nyuklia na upepo.
3. Italia – Inanunua umeme kutoka Ufaransa na Uswizi.
4. Hispania – Inanunua umeme kutoka Ufaransa.
5. Uholanzi – Inanunua umeme kutoka Ujerumani na Ubelgiji.

ASIA

1. India – Inanunua umeme kutoka Bhutan, ambayo inazalisha umeme mwingi wa maji.
2. Bangladesh – Inanunua umeme kutoka India.
3. China – Inanunua umeme kutoka Urusi na nchi jirani kama Laos kupitia mikataba ya nishati.

AMERIKA

1. Marekani – Inanunua umeme kutoka Kanada, hasa umeme wa maji kutoka Quebec.
2. Mexico – Inanunua umeme kutoka Marekani.
3. Brazil – Inanunua umeme kutoka Paraguay kupitia bwawa la Itaipu Dam.
4. Chile – Inanunua umeme kutoka Argentina.

Kwa hiyo, ununuzi wa umeme kati ya nchi ni jambo la kawaida duniani, hasa kwa nchi ambazo hazina vyanzo vya kutosha au zinatafuta umeme wa gharama nafuu kutoka nchi jirani.

Mwisho wa Kukopi na kupesti

ASSIGNMENT: kwa kutumia para moja waeleze wana JF kile ambacho umejifunza kutokana na andiko hili adimu la Mwanasheria na DC Julius Mtatiro. Usitukane
Pia, Soma
Nashauri Tununue umeme mikoa yote ya mipakani kujazia Aruha,Kilimanjaro,Manyara, Mara, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Rukwa na tukinunua wa nje wa kwetu maeneo hayo tunaufanyaje?
 
Issue ya Kununua Umeme kwa Majirani hakuna Mtu anapinga Ni jambo La Kawaida ndio mana Mikoa kama Kigom, Rukwa na Kagers ilikuwa offgrid kwasbabu ya Umbali na Vyanzo vya uzalishaji ila kwa sasa yote ipo Connected kwenye Grid na Tulisheherekea kama Sehemu ya Mafanikio kuondoa Mikoa hio Offgrid

Umeme Ni National Security matter kiufupi Kucheza na Nishati ni Kucheza na Usalama wa Taifa letu ndio mana Sera za Wizara ni Kufanya Kila liwezekanalo ili tupate Energy Independence hii ndio Policy za Wizara

Kufanya Investment kubwa kama Bwawa la Mwalimu Nyerere na Kesho kuamka na kusema Kuwa gharama za Kusafirisha Umeme mpaka Upande wa northern ni ghali sana Kuliko Kununua Umeme Ethiopia sisi tutakushangaa sana sana. Tena Unataka Kununua umeme katika mazingira ambayo una Surplus kwenye Generations

Leo unataka Ufanye Ukanda wa Kaskazini utegemee umeme wa Nje ya Nchi vipi hayo mataifa unayotaka Yakuuzie kesho yakiamka yana Scarcity au Yakaingia Kwenye Vita unategemea wataendelea kukuzia?
Umeme ni Security issue ! tukinunua na hili nalo tuliangalia kwa marefu
 
Nashauri Tununue umeme mikoa yote ya mipakani kujazia Aruha,Kilimanjaro,Manyara, Mara, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Rukwa na tukinunua wa nje wa kwetu maeneo hayo tunaufanyaje?
Bonge la swali...
 
Back
Top Bottom