DC Kinondoni: Ramani haioneshi barabara zinazodaiwa kuzibwa kupisha Kanisa la Mwamposa

DC Kinondoni: Ramani haioneshi barabara zinazodaiwa kuzibwa kupisha Kanisa la Mwamposa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-07-01 at 16.41.35_f80747db.jpg
Baadhi ya Wananchi wanaoishi jirani na eneo ambako limejengwa Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Apostle Boniface Mwamposa, wamewasilisha malalamiko yao wakidai kuwa ujenzi wa miundombinu ya kanisa hilo umesababisha changamoto ya upatikanaji wa maji na kuzibwa kwa baadhi ya njia walizokuwa wakizitumia.

Ilivyokuwa hoja ya awali ~ Wananchi Kawe: Ujenzi wa Kanisa la Mwamposa umetusababishia kukosa Maji na kufungiwa barabara

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amesema baada ya kufanya tathmini kwa kupitia nyaraka na kupata maelezo mbalimbali, amebainika katika eneo linalolalamikiwa kwa madai ya barabara kuzibwa, ramani haioneshi kuwepo kwa barabara.

Amesema kwamba licha ya barabara hiyo kutumika kwa muda mrefu na Wananchi, haipo rasmi kwenye ramani. Hata hivyo, amesema kwa busara za pamoja kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na uongozi wa Kanisa la Mwamposa, wataangalia uwezekano wa kuweka njia kwa ajili ya Wananchi kupita, na pia kuruhusu Watoto kutumia baadhi ya maeneo kwa michezo.
photo_2025-07-02_11-35-33.jpg

photo_2025-07-01_13-10-30.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akifafanua jambo.
photo_2025-07-02_11-35-37.jpg

Mhandisi Erasto Mwakilulele kutoka DAWASA Kawe
​
Mwakilishi wa Kanisa la Arise and Shine, akizungumza kwa niaba ya Mwamposa, amesema kuwa wataacha njia moja kupitika kati ya maeneo yanayolalamikiwa. Kuhusu eneo lililotumika kwa michezo, amesema kwa siku za ibada na matukio mengine, eneo hilo litakuwa likitumika kama sehemu ya maegesho ya magari.

Hata hivyo, siku ambazo hakutakuwa na matukio, eneo hilo litaruhusiwa kutumika kwa michezo kama ilivyokuwa awali.

Kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji iliyosababishwa na kuharibika kwa baadhi ya miundombinu wakati wa ujenzi wa kanisa hilo, Mhandisi Erasto Mwakilulele kutoka DAWASA Kawe, mbele ya Mkuu wa Wilaya, amesema mamlaka imepokea taarifa ya tatizo hilo na tayari wameshaanza kazi ya kuboresha miundombinu ili huduma ya maji irejee haraka kwa Wananchi.

Hata hivyo kumekuwepo na madai ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wananchi na wadau kuwa ujenzi wa Kanisa hilo kando na Shule tatu kunaweza kuathiri Wanafunzi.
 
Mwamposa anampigia sa100 debe kanisani kwake kwa hiyo msitegemee kuwa Mwamposa atasumbuliwa kwa lolote. Tulieni tu
 
Ukitaka kujua ukweli wa ramani, kesho nabii aoteshwe kuhusu wasiojulikana. Kisha akemee utekaji na kubinywa kwa haki. Hapo ndiyo utasikia amevamia barabara na kuingia eneo la bahari. Si ajabu ukasikia si Mtanzania. Anafanya kazi bila kibali🤣🤣
 
Eti baada ya kufanya tathmini ..hakuna lolote hapo na zaidi hao wananchi watulie tu waendelee na maisha yako, huyo tapeli hawatamuweza na mazombi yake yataungana kumtetea Hadi KIFO.
 
Kwakuwa hajainanga SERIKALI, hapo hana baya, sasa siku aiseme serikali, ataambiwa hapo ndipo kuna kitovu cha baba wa taifa 😂🤣
 
Amekodishwa na nilisikia hilo eneo linataka kuendelezwa na serikali sijui imefikia wapi
Linaendelezwa la huku mbele kuliko jengwa zile apartments na la nyuma yake, sema jamaa katia bonge moja la uwekezaji na jmos ya kesho ndio panazinduliwa. Huku Mwamposa, huku aeabasaba, kimbembe cha usafiri hapo sipatii picha
 
Ukitaka kujua ukweli wa ramani, kesho nabii aoteshwe kuhusu wasiojulikana. Kisha akemee utekaji na kubinywa kwa haki. Hapo ndiyo utasikia amevamia barabara na kuingia eneo la bahari. Si ajabu ukasikia si Mtanzania. Anafanya kazi bila kibali🤣🤣
Uko sahihi mkuu Niliposoma haraharaka kichwa cha habari nikahisi linazungumziwa kanisan la Gwajima.
 
Back
Top Bottom