Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Alhaji Majdi Mwanga, ametishia kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi watakaoshindwa kuwapeleka shuleni watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Mwanga alisema hayo mjini hapa katika mkutano wa hadhara na wananchi kuhusu uhamasishaji shughuli za maendeleo ikiwamo sekta ya elimu.
Alisema ili kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kidato cha kwanza wanaingia madarasani Januari 17, mwaka huu, ofisi yake imeandaa mikataba kati ya wazazi, walezi kuhusu kudhibiti tabia ya baadhi ya wazazi kuwa chanzo cha wanafunzi kukatisha masomo.
Alisema hatua hiyo ni kutekeleza ibara ya 11 (2) na (3) ya Katiba inayosisitiza haki ya msingi ya kupata elimu.
“Tumeshatayarisha mikataba ambayo inalenga kuimarisha usimamizi kwa wazazi na walezi, kutimiza wajibu wa malezi kwa watoto wao na ilishasambazwa katika shule za sekondari na ofisi za serikali za vijiji na kata,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilosa, Ameir Mbaraka, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wilaya ya Kilosa Sh. bilioni 4.3 zilizotumika kwenye ujenzi wa vyumba 186 vya madarasa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya hiyo, Kisena Mabuba, alisema jumla ya wanafunzi 9,405 ambao wanatarajia kuanza masomo ya kidato cha kwanza Januari 17, mwaka huu.
Mabuba alisema mpango mwingine ni kuhamasisha uandikishwaji wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kutoka kwenye jamii za wafugaji.
“Nawataka jamii ya wafugaji wajitokeze kuwaandikisha watoto wao waliofikia umri wa kuanzikishwa shule ili waepuke mkono wa sheria,” alisema Mabuba.
Pia alisema halmashauri itaendeleza mchakato kusajili shule shikizi, ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa shule za msingi kuondokana na ulazima wa kutembea umbali mrefu.
NIPASHE