Dc Lushoto kufanya msako nyumba kwa nyumba kuwasaka wanaotorosha watoto mashuleni

Dc Lushoto kufanya msako nyumba kwa nyumba kuwasaka wanaotorosha watoto mashuleni

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Serikali wilayani Lushoto imeanzisha oparesheni kabambe ya nyumba kwa nyumba inayolenga kuwasaka baadhi ya watu wanaoshiriki vitendo vya kuwatorosha watoto hususani wanafunzi ili kwenda kufanya kazi za ndani nchini Kenya.

Baadhi ya watoto hao ni wale walio katika shule za msingi na sekondari ambapo baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwaachisha masomo na kisha kuwapeleka Mjini Mombasa na maeneo mbalimbali hapa nchini ili kujipatia ujira kwa kazi za ndani.

Agizo hilo limetolewa Mkuu wa Wilaya ya
Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro katika kikao cha wadau wa elimu kata ya Mponde katika halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga.

Katika kikao hicho Lazaro amewaagiza wenyeviti na Watendaji wa vijiji Wilayani humo kufanya msako mkali wa kuwakamata wazazi na walezi wanaoshiriki vitendo hivyo.

“Baadhi yao wamekuwa wakiwatorosha watoto wao wa shule kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani Mombasa na maeneo mengine hii haikubaliki “alisema Lazaro

Hatahivyo,alisisitiza kwamba watoto hususani wanafunzi wana haki ya kupata elimu na kuonya kuwa watachukua hatua kali kwa wale watakaokamatwa kwenye oparesheni hiyo.

Mwisho.

66437243-97F3-4D6A-93BD-9F13B1C9B8AF.jpeg
 
Kijana anaandika Barua ya kuacha shule akavue samaki ili ajikimu kimaisha anageuzwa kituko nchi nzima

Anatakiwa arudi shule ya Kata akasome kivumi kishirikishi na akakae miaka minne amalize afeli halafu asimangwe na Wanasiasa kwanini hajiajiri

Watu wanaamua kuachana na mashule kwa kuwa kijana alieshia la saba na wa form four hawana tofauti zaid ya vyeti tu wanavyomiliki ila wote wapo Kijiweni wanaendesha boda boda
 
Kijana anaandika Barua ya kuacha shule akavue samaki ili ajikimu kimaisha anageuzwa kituko nchi nzima

Anatakiwa arudi shule ya Kata akasome kivumi kishirikishi na akakae miaka minne amalize afeli halafu asimangwe na Wanasiasa kwanini hajiajiri
Kabisa,sio kila mtu kaumbiwa elimu.
 
Wanataka kila mtu awe na index no.ya form 4 kama kitambulisho cha Taifa

Nakaa na vijana wengi wa form four hizi za oya oya sioni tofauti yao na wale wa la saba
Kabisa,sio kila mtu kaumbiwa elimu.
 
Wanataka kila mtu awe na index no.ya form 4 kama kitambulisho cha Taifa

Nakaa na vijana wengi wa form four hizi za oya oya sioni tofauti yao na wale wa la saba
Na ni mjini. Elimu ya darasani inataka uwezo wa ku-imagine.

Ila uongozi ukiwa na nia ya kuleta maendeleo ni mgumu sana. Yaani hao pia unatakiwa ufanye mipango kwa ajili ya mustakabali(future) wao. Ili waondoke kwenye umasikini.
 
Back
Top Bottom