MPOGOLO: ATAYETUPA UCHAFU JIJINI DAR FAINI LAKI 3 HADI MILIONI 1 AU KIFUNGO CHA MIEZI 12–24
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amesema mtu atakayebainika kutupa taka hovyo jijini Dar es Salaam atatozwa faini ya shilingi 300,000 hadi milioni moja au kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 hadi 24, kwa mujibu wa Kifungu cha 41 cha Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024 (GN Na. 1011).
Akizungumza Septemba 19, 2026, baada ya kuhitimisha zoezi la usafi wa mazingira jijini, Mpogolo amesema sheria hiyo imeanza kutekelezwa kikamilifu ili kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi, salama na yenye mazingira bora.
Amesema Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi, lakini hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaotupa taka hovyo, kutiririsha maji au kufanya vitendo vingine vinavyokiuka sheria za usafi na mazingira.
Mpogolo amesema utekelezaji huo haulengi adhabu pekee, bali kujenga nidhamu, uwajibikaji na utamaduni wa usafi. Halmashauri pia itaendelea kuweka maeneo na vifaa vya kuhifadhia taka, pamoja na kuhamasisha utenganishaji wa taka kulingana na aina zake.
Ili kuimarisha ufuatiliaji, Jiji limejipanga kuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya JKT na kuwapatia vyombo vya usafiri kwa ajili ya kusimamia usafi mtaa kwa mtaa.
Aidha, amesema barabara zote muhimu za Jiji, maarufu kama Smart Roads, zitasimamiwa kikamilifu ili zibaki safi, zipandwe miti rafiki na salama, na ziendelee kulipamba Jiji.
Amesema biashara katika barabara hizo hazitaruhusiwa bila kibali cha Mkurugenzi wa Jiji, huku wafanyabiashara wakitakiwa kufanya shughuli zao katika maeneo yaliyopangwa. Hatua hiyo inalenga kupunguza mson.
Pia soma
~ Watu wanatupa taka nyingi kwenye mabonde ya mito. Hiyo ni mbaya kwa afya na mazingira
~ Dar: Viongozi wana mpango gani na usafi wa mazingira? Maeneo mengi ni machafu, hakuna mkakati wa wazi unaotekelezwa
~ Huu uchafu mtaroni hapa Sinza Africasana, wahusika hawauoni au hakuna wa kuwajibika?
~ Dar: Mtaa wa kidosho - Mikocheni uchafuzi wa daraja linalopitisha maji taka ni chanzo cha malaria
~ Dar es Salaam: Mtaa wa Darajani - Mikocheni A, maji ya kinyesi yanasambaa tu mtaani
~ Watu wanatupa taka nyingi kwenye mabonde ya mito. Hiyo ni mbaya kwa afya na mazingira
~ Hizi mvua na mrundikano wa taka maeneo mengi ya Dar, mamlaka hazioni hatari ya kipindupindu?
~ Mwenge: Uchafu unarundikwa holela kwa muda mrefu pembezoni mwa makutano ya barabara; mamlaka zipo wapi?
~ Mitaro ya maji Kawe Ukwamani (Dar) imeziba kwa uchafu unaotoa harufu mbaya, Maafisa Mazingira Kinondoni wako wapi?
Hoja nyingine:
- Kituo cha Gongo la Mboto A na B: Taka zalundikwa Barabarani, zinaleta uharibifu wa barabara na kuhatarisha Afya za Watu
- Kusuasua kwa uzoaji taka kunatishia Afya za wakazi wa Ubungo Riverside
- Hali ya fukwe za Bahari Mbezi Beach (Jangwani) haziridhishi; Tutaenda na hali hii AFCON?
- Huu uchafu mtaroni hapa Sinza Africasana, wahusika hawauoni au hakuna wa kuwajibika?