Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na TARURA imeanza utekelezaji wa ukarabati wa barabara ya Tabata Bima–Kimanga iliyopo wilaya ya Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu na kuondoa changamoto ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo, hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema tayari Serikali imepokea fedha kutoka kwa Rais, Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa Mita 650 unaolenga kujengwa kwa kiwango cha zege.