DC Mstaafu Simon Odunga akosoa vikali jinsi Kumbukumbu ya Hayati Magufuli ilivyofanyika

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Simon Odunga amekosoa kitendo shughuli ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati JPM Serikali kutuma mwakilishi kwenye tukio hilo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Waziri Bashungwa Mkuu huyo wa Wilaya Mstaafu amesema nanukuu

"Suala la JPM halikuwa na hadhi ya kutuma mwakilishi Tena Waziri Hilo HAPANA. Palitakiwa aidha Rais mwenyewe, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar au Makamu wake, Waziri Mkuu au Rais Mstaafu tofauti na hapo suala hili halijapewa portfolio inayokubalika na nasema waziwazi mwambieni Mheshimiwa Rais hajatutendea Haki na ametuudhi Sana Wana CCM na asifikiri maridhiano yake yanatuhusu hayo ni yake na tutabaki kuwa mahafidhina"

Mwisho wa kunukuu.
 
mbona kama ana hoja wajuzi kina Pascal Mayalla hebu mje mtuongezee maarifa. kuhusu kauli ya mstaafu DC
 
nasema waziwazi mwambieni Mheshimiwa Rais hajatutendea Haki na ametuudhi Sana Wana CCM na asifikiri maridhiano yake yanatuhusu hayo ni yake na tutabaki kuwa mahafidhina
Wana CCM walioudhika ni wepi ndugu unaowazungumzia? watakuja kukukana kwamba hawajakutuma kusema hayo na wewe sio msemaje wa wana ccm hata kama hoja yako ni nzuri
 
Watanzania ni watu ambao wako bsy kubishana na kupigania mambo ya kipuuzi.
Hayo mambo ya kumbukumbu yabaki kuwa ya kifamilia na ambaye atataka kwenda. Sasa wanataka eti raisi aende naye anawachora tu...
Hayo Mambo ya familya pia kwenda chato haimaniishi ndo unakuwa umemkumbuka ni SAwa na mtu anayelia msibani haimaniishi Msiba umemgusa
 
Duh

...sukuma gang!
Muda mwingine lazima ukweli usemwe. Mimi huwa nakubaliana na raisi Samia kwa mambo mengi, na pia sipo upande unaoitwa wa Sukuma gang.

Lakini kwa yaliotokea siku hii muhimu ya kumbukumbu ya raisi aliekuwa tayari kuweka maisha yake rehani kwa ajili ya watanzania wote.

Nasema hapana aisee. Serikali imechemsha na ni bora swala hili wangelitolea maelezo yanayoeleweka.
 

Mama samiah hapendi unafiki
 
Wazee inatosha sana haina haja ya kuleta malumbano na kuja kuleta machafuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…