Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amelazimika kumpigia simu Meneja wa Wakala wa barabara Vijijini TARURA mbele ya wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kupata ufafanuzi juu ya ujenzi wa barabara iliyopo katika kijiji cha Shatimba kata ya Nyamalogo halmashauri ya Shinyanga.
Hayo yamebainika katika ziara ya kikazi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndani ya halmashauri hiyo ambapo DC Mtatiro amemuagiza meneja wa TARURA kufanya uchambuzi wa barabara hiyo haraka iwezekanavyo kutokana na kuwa kero kwa wananchi.
Wakizungumza na Wasafi Media mara baada ya mkutano wa hadhara baadhi ya wakazi na viongozi wa kata ya Nyamalogo wamekiri uwepo wa changamoto ya miundombinu ya barabara hususa ni katika kipindi cha mvua za masika hali inayopelekea wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao.
"Miundombinu kwenye eneo letu sio rafiki ni kwasababu tuna barabara moja ambayo ilichongwa lakini imeshakatika kwa upande wa kijiji cha Shatimba barabara ni mbovu sana hususa ni katika kipindi hiki cha masika, wakulima na wanafunzi wanaosoma ng'ambo ya barabara kushindwa kuvuka, tunashukuru leo hii mkuu wa wilaya amefika na kujionea mwenyewe na kutoa maelekezo kwa mamlaka zinazohusika kuchukuwa hatua za haraka", amesema Diwani Silas Cheo