DC Mtatiro: Marufuku kufanya Sherehe za darasa la saba, fedha za Sherehe wazitumie kuwasomesha wasiwe mzigo kwa Taifa

DC Mtatiro: Marufuku kufanya Sherehe za darasa la saba, fedha za Sherehe wazitumie kuwasomesha wasiwe mzigo kwa Taifa

socrates alisema golden brain wawe watwala silver wawe walimu iron wawe askari kwa nchi yetu iron ni watawala silver ni walimu na golden ni askari. matokeo yake ndo kama hayo. ccm ni janga la taifa penda usi pende huu ndo ukweli
 
Hivi huu wivu wa kijinga wa watu wazima kwa watoto tumeutoa wapi...!

Sherehe ya masaa manne tu Serikali ya tunduru inaathirika vipi...!

Nilishangaa mmoja alipopiga marufuku majoho kwa baadhi ya sherehe badala ya kutofautisha rangi na design ya hayo majoho kwani hata chekechea akivaa hapunguzi kitu ikiwa wazazi wake wameridhia bila shurti ashiriki.

Sent using Jamii Forums mobile app
uwezo wake mdogo sana baada ya kuhamia ccm
 
Yaani wazazi kufanya graduation kwa watoto wao tena kwa gharama zao leo imekuwa kosa!, kufanya graduation sio kudumaza mtoto, kwangu ni kum_motivate aende mbali zaidi, kwamba baby umemaliza level hii now unakwenda stage ya pili sawa?, yes daddy!, it's like that my friend Mtatiro, km wewe unalea wanao kibaunsa ok, but wengine tunawalea fresh tu, story , utani, nn, poa tu... unaogopa kumvalisha mtoto joho? hebu wacha ushamba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufanya sherehe kwa kila hatua ya uhitimu wa masomo ni hiari ya mtu na asizuiwe.

#KaziNaBata
Hivi kwenye eneo ambalo mimba utotoni na utoro ni mkubwa vile nadhani ni muhimu kwa wazazi wana haki yakuwapingeza watoto wao kwa kuhitimu....huu mtindo wa kuongea bila kutafakari una madhara makubwa Kama huku
Mjini tunawaoingeza watoto wetu kwa kuwawekea sherehe kubwa majimbani why huko huko vijijini...na ikumbukwe kuwa huo ndo Muda mrefu zaidi almost nusu ya maisha ya shule yanaishia primary
 
Sasa huku ni kuingilia uhuru binafsi wa watu.
Kama mtu anataka kufurahia hatua yake ya kumaliza la saba wewe ni nani hadi umzuie?
 
Mkulu akichemka tunasingizia washauri na wasaidizi wake wa chini. Hivi wakuu wa mikoa na wilaya pia wanawashauri tuwasingizie wao pia ????

Kinachofanyaka hivi sasa ni zaidi ya kusherekea za kumaliza STD VII. Hizi graduation ni sehemu ya kujenga na kudumisha mahusiano baina ya wazazi, jamii na shule.

Pia ni sehemu ya kuwatia moyo wanafunzi na wazazi mtoto anapoanza chekechea anapaswa kufika darasa la 7 na kuendelea hasa wilaya ya huyu mh ya Tunduru ambako suala la elimu ni kitendawi, watoto wengi hawafiki hata darasa la 7 kwa sababu ya mimba na unyago.

Nimshauri mkuu wangu wa wilaya afuate nyayo za msaidizi wake Homela ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa katavi. Mbali ya kusukuma maendeleo ya elimu alicheza sana na media. Mfano, aliwachezesha wayao ngoma mchana kweupe kumsifia mkulu km masihi au mtume kwenye sakata la korosho wakati hata senti moja walikuwa hawanyalipwa.

Jambo asilojua mkuu wangu Mtatiro bila kumsifia mkulu hatoboi! Mission ya CCM completed kilichobaki ukubali kucheza iyena iyena ndiyo salama yako. Mungu ibariki Tz, Mung u ibariki Afrika
 
Kweli ccm inaharibu akili za watu, mtatiro sio wa kuongea vitu vya kipuuzi hivi.
 
Sijui ni mimi tu nawaza hivi,hivi ni kwanini mtu hata kama alikuwa na akili timamu,akipewa tu uDC akili zinatoweka ghafla
 
Huyu jamaa nimemsikia leo nimemdharau sana mbona yeye pamoja na degree yake lakini bado anajinyenyekeza kwa ma boss wake? Huyo ni mshamba tu kama walivyo washamba wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom