DC mteule ndugu "Mchopanga" alisoma shahada ya kwanza bila kuwa na matokeo ya kidato cha sita licha ya kuisoma kwa miaka mitatu

DC mteule ndugu "Mchopanga" alisoma shahada ya kwanza bila kuwa na matokeo ya kidato cha sita licha ya kuisoma kwa miaka mitatu

Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka...
Hilo si jukumu la nacte bali tcu.
 
Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka...
Bado unazungumzia elimu kwenye u dc mkuu angalia zifa nyingine za ziada! Sifa hizo za ziada kama u sanii ndoo umembeba kufika hapo alipo. Kwani wewe kwa maoni yako dc anatakiwa awe na elimu gani na wapi imeandikwa kwenye sheria za utumishi wa umma
 
Kama ingekuwa form 6 lazima.... waliosoma kenya wote.. ama wakenya wasingekuwa na degree holder hata mmoja?

Unajua kuna wakenya kibao wamesoma udsm wakina miguna miguna na jaji mkuu wao ila kenya hawakusoma form 6 sababu haipo kwao.

Pia unajua kujua michezo kama soka, basketball, riadha inaweza kukupa nafasi ya kusoma havard ama yale bila kujali hujafika form 6 wala nini?
Kenya wanasoma hadi darasa la nane na degree wanasoma miaka minne.

Kenya. 8+4+4=16
Tanzania 7+4+2+3=16
 
Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka..
Kwani Hata akiwa na PhD ndio itakayo kuwa DC!? Achen ushamba wa kutukuza vyeti ambavyo wengine wanavyo kwa kuvua chupi kwa prof. Tunahitaji watu wenye skills za uongozi sio wenye vyeti.
 
Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka...
Mkuu teuzi Kama teuzi , mh Rais mteuwe SAIDA KALOLI,pitia wimbo wake wa chambua Kama kalanga ,anafaa ,naona UDC umekua Kama wimbo wake ,wa chambua Kama karanga
 
Kenya wanasoma hadi darasa la nane na degree wanasoma miaka minne.

Kenya. 8+4+4=16
Tanzania 7+4+2+3=16
Apo ongeza miaka tena miwili kwa medical student na mwaka mmoja kwa engeneering kozi kwa tanzania
 
Apo ongeza miaka tena miwili kwa medical student na mwaka mmoja kwa engeneering kozi kwa tanzania
Ukiona imeongezeka kwetu na kule ni hivyo hivyo. Sio kwamba Kenya medical pia wanasoma miaka minne hiyo hiyo
 
Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka...
Nisichokielewa Ni uteuzi pendwa Kuna PhD holders na Ngumbaru wenzetu. Wanaangalia nn haswa?
 
Fuatilia, utajua na kuelewa vizuri Kabisaa.

Jibu swali maana unaongea uongo.. hata vyuo vya kenya zipo degree kibao za miaka mitatu kama udsm na wakenya wanazisoma hizo za 3 yrs.

Unajua university of nairobi na university of dar es salaam zilikuwa colleges za university moja kubwa inaitwa university of east africa? Chini ya management moja.

Kozi nyingi ambazo udsm ni 3 yrs na nairobi ni 3 yrs hivyo hivyo
 
Huna pesa ya kusoma nje ya nchi wewe

Hakuna mtanzania asiyependa mwanae akasome Oxford, University of london

Ada ni kubwa wenzetu wahindi wamewekeza kumlipia mtoto wa chekechea dollar 30,000 Marekani ni kawaida sana...
Yote uliyoandika hayaondoi ukweli si kila chuo cha nje cheti chake kinakubalika hapa nchini.
 
Mnashangaa kitu gani?

Kwani kusoma chuo kikuu mpaka usome Form Six?...
Kwani yeye ni mhindi.

Kwa mfumo wa Tanzania Kuna njia mbili tu za kupata elimu ya chuo kikuu.

Direct qualifications (form 6) na Equivalent qualifications.

Sasa yeye alienda kusoma kwa kupitia route gani? Utaratibu wa degree za huko India ni upi?
 
Jibu swali maana unaongea uongo.. hata vyuo vya kenya zipo degree kibao za miaka mitatu kama udsm na wakenya wanazisoma hizo za 3 yrs...
Siwezi kuongea kitu ambacho sina uhakika nacho kwa sababu sina data za wala sijui sifa za hao wadahiliwa.

As long as criterias za admission ni zaidi ya moja. Kwa hiyo sina muda wa kushangaza ni kwa jinsi gani wakenya wanasoma hapa kwetu.

Pia ukitaka kujua kuwa mambo ni tofauti jaribu kutumia cheti cha form four cha hapa Tanzania kuomba University kule Kenya.

Suala la kusema naongea uongo hilo ni juu yako na hekima zako
 
Kwani yeye ni mhindi.
Kwa mfumo wa Tanzania Kuna njia mbili tu za kupata elimu ya chuo kikuu,
Direct qualifications (form 6) na Equivalent qualifications.
Sasa yeye alienda kusoma kwa kupitia route gani? Utaratibu wa degree za huko India ni upi?
Ni utaratibu kwa wewe maskini usiye na Pesa

Ukiwa na pesa kuna shule kibao Tanzania zinatumia mifumo ya cambridge

Maskini ndio hao wanasoma udsm, Dodoma university

Ukiwa na pesa au dollar huwezi somesha mtoto Tanzania, Ni Umaskini wa watanzania

Mkuu watu wanaokuzunguka wana pesa za kutosha, Angalia aina za marafiki zako

Uelewa wako wa elimu unaishia TCU

Huo mfumo upo kwa ajili ya watoto wa maskini

Mtoto wako kusoma udsm au Udom sio sifa, Wazee wetu walisoma hapo hawakuwa na pesa

Leo hii watu wana pesa, Ukiwa na pesa huwezi mkaririsha mtoto mambo
 
Back
Top Bottom