DC mteule ndugu "Mchopanga" alisoma shahada ya kwanza bila kuwa na matokeo ya kidato cha sita licha ya kuisoma kwa miaka mitatu

Sitaki utaje vitu unavyomiliki ewe msomi. Mbona mgumu kuelewa? Halafu usijichekeshe chekeshe kuua soo.

Wewe si msomi, nataka utueleze nini umefanya kinachokutofautisha wewe na elimu feki ya Mchopanga.
Mimi sijipendekezi kutafuta teuzi kama Mchopanga. Elimu yangu imenipa uhuru.
 
Mimi sijipendekezi kutafuta teuzi kama Mchopanga. Elimu yangu imenipa uhuru.
Wewe na Mchopanga nani yuko huru zaidi?

Kwa taarifa yako Mchopanga ndiye msomi zaidi kuliko wewe uliyepita form 6 na kwenda chuo.

Amekuwa huru kiasi kwamba akaweza kuchangamana na wakubwa mpk ameteuliwa kuwa DC.

Sasa yuko huru kifikra, kijamii na atakuwa huru zaidi kiuchumi baada ya kupata uDC.

Mkaruka vipi mkuu? Huwezi kuwa huru kama una njaa ya tumboni ama mfukoni.
 
Nani kakwambia mimi nina njaa ?

Mwenye njaa yuko huko anazurula na kutoa toa macho huku akisifia wanaume huko Lumumba kutafuta chochote.

Mimi ni complete free human creature.
 
U-DC hauna haja ya aina hiyo ya cheti!! ni swala la kujua kusoma na kuandika tu!! rejea awamu ya tano
 
Mimi ni complete free human creature.
Kama ni kweli upo free, basi jiepushe na mijadala ya kulaumu akina Mchopanga. Wanaolaumu wanateswa na mzimu wa kukosa uteuzi ili watibu njaa zao. Maana hawana hoja za msingi.
 
Kama ni kweli upo free, basi jiepushe na mijadala ya kulaumu akina Mchopanga. Wanaolaumu wanateswa na mzimu wa kukosa uteuzi ili watibu njaa zao. Maana hawana hoja za msingi.
Wewe takataka, watu lazima walaumu kwasababu huyo Mchopanga haendi kufanya kazi nyumbani kwa Samia.
 
Wewe takataka, watu lazima walaumu kwasababu huyo Mchopanga haendi kufanya kazi nyumbani kwa Samia.
Usiseme watu, ukajitoa. Jiweke na wewe. Lkn hoja yangu ni kwamba toeni sababu za msingi. Vinginevyo mnadhalilika tu hapa.

Mwenzenu anashona suti akijiandaa kuapishwa. Huku mnaojiita wasomi mliopitia form 6 Kisha mkaenda vyuo mkitokwa povu midomoni.
 
Dunia ya leo imeisha badilika tukubali pia kubadili mifumo yetu ya elimu ili kuendana na wakati na mahitaji ya sasa suala la form six siyo kigezo wala maana wapo pia watu wananzia huku chini na wanafanya vizuri tu
 
Hata mm naona ni ujinga kupuuza elimu ya mtu sabb tu hakusoma form 6. Elimu kazi yake kubwa ni kumpatia mtu maarifa. Sasa hao wanaolaumu wanamaanisha kwamba maarifa yote ktk mfumo wa elimu yako form 6 ?

Au mtu akipata maarifa bila ya kupita form 6, maarifa hayo huyeyuka? Ni ujinga.
 
hoja ni nini mbona huko nyuma watu walikuwa wanatoka direct form four kwenda chuo kikuu na kufanya vizuri.labda ungesema hakufannya vizuri kidato cha nne hapo kuna hoja lkn kama alikuwa na credit nne mimi sioni hoja.
 
Mkuu degree yake haitatusaidia hata Ndugai ana masters, tuna taka utendaji kazi uliotukuka na siyo vyeti
 
Ndugai ana masters analisaidia nini taifa? elimu ya bongo nayo ni elimu?
 
hoja ni nini mbona huko nyuma watu walikuwa wanatoka direct form four kwenda chuo kikuu na kufanya vizuri.labda ungesema hakufannya vizuri kidato cha nne hapo kuna hoja lkn kama alikuwa na credit nne mimi sioni hoja.
Kabudi ni Professor amesaidia nini nchi? elimu zao hazina faida yoyote kwa taifa.
 
Form four yetu hii ya NECTA haina sifa ya kuku bridge kwenda University dunia nzima. Isipokuwa tu kama utapitia kwenye program maalumu ili ikuongezee sifa au Utaspend muda zaidi ya wenzako kwenye course yako.

Jaribu kuomba admission ya chuo kikuu hapo Kenya kwa matokeo yako ya form four ili usome degree. Halafu lete mrejesho hapa.
 
Elimu ya secondary haifundishi utaalamu wowote, kwahiyo ni vizuri kuwa na elimu ya chuo ya muda mrefu na secondary muda mfupi. Maana sehemu kubwa ya kazi tunatumia elimu ya chuo.
Vizuri.

Ila hii hoja yako ina tofauti na mada ndogo ya mazungumzo yetu.

Tanzania tuna bahati kwa sababu tuna mifumo yote miwili. Hii ni fursa nzuri kwetu.
 
Nimekuelewa vizuri sana but mfano wako wa Kenya HAPANA, ni kweli Kenya wanaishia form 5 but remember wao msingi wanakwenda hadi darasa la nane so kimsingi ni kama masomo ya form 1 kwao ndio darasa la nane, by numbers miaka ya kukaa shule ya Kenya na Tanzania or Uganda ni sawa tu. Mengine nakuunga mkono but edit hapo tu
 
Kenya ni nchi ambayo haina system ya kidato cha sita. chi nyingine ni Afrika Kusini (Ina vidato vitano). Unasemaje juu ya hilo? Pia kuna nchi zingine huwa zina bridging programme za mwaka mmoja kwa wale wanaotaka kusoma shahada za kwanza, unasemaje juu ya hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…