DC Muro avuruga mtandao wa wizi wa ng’ombe za watu majumbani

DC Muro avuruga mtandao wa wizi wa ng’ombe za watu majumbani

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Mkuu wa wilaya ya Arumeru , Jerry C. Muro ametumia saa 18 kusambaratisha mtandao wa wizi wa ng’ombe za wananchi majumbani ambapo mpaka sasa watuhumiwa 5 sugu wa wizi wa ng’ombe tayari wako mikononi mwa vyombo vya dola.

Dc Muro amelazimika kuingilia kati baada ya ng’ombe zaidi ya 13 kuibwa kwa mbinu za wezi kuvamia majumba ya watu alfajiri na kuvunja milango ya mabanda na kutoa ng’ombe na kwenda kuzichinja katika shamba la Gomba na kandokando ya barabara ya By pass na kisha kuondoka na nyama ambazo huzipeleka mabuchani mjini asubuhi na kuwaachia wananchi hao ng’ozi.

Katika kikao cha hadhara ambacho kiliitishwa kilibainika kuwepo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakishirikiana na wahalifu kutoka nje ya wilaya ambao wanapewa ramani ya nyumba zipi zenye ng’ombe wanaofaa kuchinjwa na kisha wahalifu kuvamia nyumba hizo.

Mara baada ya kikao hicho DC Muro na baadho ya askari walianza msako na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 5 ambao wanaendelea kushikiliwa na vyombo vya dola kwa hatua zaidi.
 
Back
Top Bottom