GE2025 DC Mwaipaya aongoza Wananchi na Vyombo vya Usalama katika matembezi ya miguu

GE2025 DC Mwaipaya aongoza Wananchi na Vyombo vya Usalama katika matembezi ya miguu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya, Oktoba 24,2025 ameongoza vyombo vya ulinzi na usalama, wananchi na vikundi mbalimbali vya Jogging na hamasa katika matembezi ya miguu kuzunguka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mtwara Mikindani. Matembezi hayo ya miguu yalihudhuriwa na Kamanda wa Brigedi ya 401KV Kanda ya Kusini Meja Generali Charles Feruzi.

1761374737882.png
Akizungumza baada ya matembezi hayo Mwaipaya amewapongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kujumuika pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha umoja na mshikamano baina ya vyombo hiyo. Pia amevipongeza vikundi vya Jogging na hamasa kwa kuungana na vyombo vya ulinzi katika matembezi ya miguu.

1761374789427.png

Aidha Meja Jenerali Feruzi amewapongeza na kutoa zawadi kwa baadhi ya wazee wa kikundi cha Likonde Jogging walioshiriki katika matembezi hayo.

1761374778083.png

1761374806608.png

1761374816573.png
 
Wameanza kuandamana kabla ya muda. Hivi kama hayo maandamano hamyaogopi mnatembea in public kutishia watu ili iweje?
 
Back
Top Bottom