Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwangwala amepongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha kampeni hiyo, huku akibainisha kuwa polisi wa sasa ni tofauti na wa zamani.
“Polisi wa sasa si tu wa kukamata wahalifu, bali wanatoa msaada wa kisheria, elimu, na kuwaunganisha watoto wanaokumbwa na changamoto na taasisi zinazoweza kuwasaidia,” alisema Mwangwala.
Aidha, alieleza kuwa jamii inapaswa kuanza na familia katika kutokomeza ukatili huo, akisisitiza kuwa malezi ya watoto yamepungua kutokana na wazazi kuweka msisitizo zaidi kwenye uchumi kuliko maadili.
Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abel Mtagwa, alisema wazazi wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kujenga jamii bora.
“Baba na mama tuungane kumkemea mtoto kwa pamoja ili tujenge kesho yetu. Bila mshikamano huu, majirani hawawezi kuingilia kusaidia kama wazazi wenyewe hawako imara,” alisema Mtagwa.
Naye Mrakibu wa Polisi, Asia Matauka, ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kilimanjaro, alieleza kuwa bado juhudi zaidi zinahitajika katika kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia.
“Lengo kuu la kampeni ya "Tuwambie kabla hawajaharibiwa" ni kuhakikisha tunatokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,” alisema Matauka.
Kampeni hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya jeshi la polisi na jamii katika kupambana na ukatili wa kijinsia, hasa kwa watoto, kwa kuhakikisha wanaelimishwa na kupatiwa msaada unaostahili.
Uzinduzi huo ulihudhuliwa na (SACP) Kulyamo SO1 Tps, (ACP) Lazaro Mwanyasi polisi jamii mkoa wa kilimanjaro,Maocd wa wilaya zote, pamoja na Taasisi mbalimbali zikiwemo AJISO, TUSONGE, Amani Center, Courage, EFM Jogging Club, KWIECO, Coca-Cola, Kilimanjaro Water Drinking,TRA, Chuo cha Singachini na Chuo cha Wanyamapori Mweka, pamoja na kikundi cha ngoma cha Msonje.