Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZIARA YA MHE MWENDA YATOA MAJIBU YA KERO 5 NZITO IRAMBA
Akiwa siku yake ya pili ya ziara ya kuendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika kata ya Kiomboi, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Suleiman Yusuph Mwenda alipokea changamoto ya maji ambayo Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA akatoa majibu ya kero hiyo.
Mwakilishi wa Meneja wa RUWASA alimwambia Mkuu wa Wilaya Mhe Mwenda kuwa Mji wa Old Kiomboi kuna tatizo la maji na kwenye Bajeti ya 2021/22 wamepanga kujenga mtandao wa mabomba ya maji yenye thamani ya Tshs milioni 89,807,801. Pia wanatarajia kujenga tanki lenye ujazo wa cubic metre laki 5 Old Kiomboi na laki 5 nyingine Lulumba.
Pia Mhe Mwenda akaagiza Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wale wenye changamoto za kushindwa kulipia matibabu wafike Idara ya ustawi wa Jamii wapatiwe huduma.
Kuhusu changamoto ya umeme eneo la Salala, Mwakilishi wa Meneja wa Tanesco ameahidi hadi kufikia tarehe 10/08/2021 watakuwa wameweka transfoma eneo la Salala.
Suala la Mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia TASAF, baadhi ya watu wamesahaulika. Majibu yakatolewa kwamba kwenye mwaka huu mpya wa fedha 2021/22 wataendelea na zoezi la kuzitambua kaya hizo ili ziingizwe kwenyeh mpango wa kuzinusuru kaya masikini huku Mhe Mwenda akikazia sala la kuwahamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Bima wa CHF ili wasihangaike wakipata maradhi.
Pia Mhe Mkuu wa wilaya aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakikisha wananawa maji tiririka na kutumia vitakasa mikono pamoja na kuvaa barakoa.
#KaziinaendeleaIramba