DC Shaka: Hakuna atakayemwaga damu ya Mwanakilosa mwenzake tena, sio damu tu hata wa kumwaga Mkojo hapa hayupo tena-VIdeo

DC Shaka: Hakuna atakayemwaga damu ya Mwanakilosa mwenzake tena, sio damu tu hata wa kumwaga Mkojo hapa hayupo tena-VIdeo

Jesusie

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
1,543
Reaction score
791


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mhe Shaka Hamdu Shaka asema hayuko tayari chini ya Uongozi wake wa Wilaya ya Kilosa kuona Wilaya hiyo ikirudia historia yake ya nyuma,

Akiongea na Wananchi wa Kata ya Tumbatu mahali palipotokea mgogoro wa Kimipaka ngazi ya Vijiji na Vitongoji,

DC Shaka amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya Viongozi wastafuu wa Vijiji na Vitongoji wanaowatumia vijana Ili kuchoche Migogoro Wilayani hapo,

Hata hivyo, DC Shaka amewahakikishia Wananchi wa Kata ya Tumbatu na Wilayani nzima ya Kilosa kuwa chini ya Uongozi wa Rais Samia na yeye kama Mkuu wa Wilaya hiyo hakuna mtu yoyote mwenye uwezo wa kumwaga damu ya mwingine lakini anaenda mbali na kusema sio tu kumwaga damu hata wakumwaga Mkojo tu hayupo na Kilosa ni salama.

Msikilize kwà makini mpaka Mwisho hapo juu.
 
Shaka huyu alipokuwa Mwenezi alianzisha propaganda ya kuwa kuna nchi tatu zimeomba kuongozwa na Samia wanapenda aina ya uongozi wake, tumeona Wakenya wakitukana matusi ya nguoni na kumdhalilisha, Shaka ana kikundi cha propaganda za mitandaoni ikiwemo akaunti hii iliyoandika huu upumbavu !
 
Back
Top Bottom