DC Ubungo afika nyumbani kwa Damian Method anayedaiwa kutekwa na watu wenye silaha, asema uchunguzi unaendelea

DC Ubungo afika nyumbani kwa Damian Method anayedaiwa kutekwa na watu wenye silaha, asema uchunguzi unaendelea

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakuu

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Twange amefika nyumbani tarehe 03 Februari, 2025 akisema vyombo husika vinaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa Damian Method huku akiitaka familia kutoa ushirikiano mara wanapopata taarifa yoyote kuhusu tukio hilo la utekaji.

Kijana anayejulikana kwa jina la Method Damian ameripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana mnamo Februari 28, 2025, katika eneo la Sinza E, Dar es Salaam.

Soma pia: Pre GE2025 Dar: Method Damian Kumdyanko adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha

Kwa mujibu wa mzazi mwenza, Tullah Chaula, tukio hilo lilitokea ghafla, ambapo watekaji walimvamia Method Damian na kumlazimisha kuingia kwenye gari aina ya Prado nyeupe kabla ya kuondoka naye kuelekea kusikojulikana.

 
Huyo jamaa alikuwa anajishugulisha na nini???

Ova
 
Kidogo kidogo tunakuwa kama mexico. Baadaye wataanza hata kuteka na polisi
 
Kidogo kidogo tunakuwa kama mexico. Baadaye wataanza hata kuteka na polisi
Sinza kuna matukio sana kwa taarifa nliyopewaga huko ni watu wanachukuliwa sana!
Ila ningependa kujuwa huyo jamaa ni nani hasa anajiahugulisha na nini?je ni mwanaharakati,mfanyabiashara/au mtu wa dili dili/dalali

Ova
 
Back
Top Bottom