DC wa Chakechake, Zukhra: Wanahabari acheni woga, andikeni habari zenye tija

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-05-19 at 17.07.35.jpeg
Waandishi wa Habari wametakiwa wasiwe waoga bali waendelee kuandika habari zenye ukweli na zenye kuzingatia maadili, ambazo zitaleta maslahi kwa Umma.

Nasaha hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Zukhra Mgeni Othman wakati akizungumza na wandishi pamoja na wadau wa habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa Vyombo vya habari yaliyofanyika Manispaa Chakechake mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema wandishi wa habari wamekua wakikumbana na vikwazo kadhaa wakati wanapokua katika majukumu yao, hivyo wasiwe waoga wasimame penye ukweli na wandike habari zitakazoleta maslahi kwa Jamii.

‘’Tunafahamu kwamba mmekua mkipata vitisho ila msitishike isaidieni jamii, ilimradi tu muzingatie miko na maadili yenu,’’alisema.
WhatsApp Image 2026-05-19 at 17.08.26.jpeg
WhatsApp Image 2026-05-19 at 17.08.25.jpeg
Aidha aliwataka wandishi hao kuandika mema ambayo yamefanywa na Rais wa Zanzibar, wananchi wayafahamu na waweze kujipatia fursa na kuweza kufaidika nayo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Ofisa Mdhamini wizara ya Habari Adam Abdalla Said aliwasisitiza wandishi wa habari kuumwa nan chi yao kwa kuandika habari zenye maslah ya jamii, na wasishie kuandika habari za matukio tu.

‘’Ndugu zangu wandishi wa habari msishie kuandika habari za viongozi tu, bali ibueni changamoto zinazowakumba wananchi wetu na kuweza kutatuliwa,’’alisisitiza.

Mapema mkuu wa Wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja aliwaasa wandishi wa habari kuepuka kuandika habari za uongo, ambazo zitasababisha mifarakano na migongano Nchini.

‘’Siku zote jambo la uongo halina mwisho mwema, hivyo niwatake wandishi wa habari kufanya uchunguzi wa kina juu ya habari watakayoiandika, ili mwisho wa siku ikajakupelekea machafuko na kukosekana kwa amani tuliyonayo Nchini mwetu,’’aliwanasihi.

Mwenyekiti mstaafu wa Jumuia ya Wandishi wa Habari Pemba Press Club (ppc) Siad Mohammed Ali alisema Wandishi wa ahabri ndio sauti ya wanyonge hivyo ipo haja kujikita zaidi vijijini kuibua kero zilizoko ili jamii iishi ikiwa salama.

‘’Wandishi tumesahau wajibu wetu hatuendi vijijini tukasikiliza changamoto, tunaishia kujipendekeza kwa watu wenye uwezo wao,’’alisema.

Mratibu wa Shirika la Utangazaji Ofisi ya Pemba Selme Mohamed Suleiman ili wandishi wa habari waweze kufikia lengo la kuleta mabadiliko katika jamii, ni budi wawe na mashirikiano ya pamoja wakati wakiwa katika kazi zao.

Akiwasilisha mada Katibu wa Jumuia ya Wandishi wa Habari PPC Ali Mbarouk Omar alisema lengo la wandishi wa habari sio kuichafua serikali ni kuandika habari zenye uzalendo na zenye kuleta maslahi kwa jamii na Taifa kiujumla.

Nae Mrakibu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Pemba Aloyce Jakob alisema watahakikisha wanashirikiana na wandishi wa habari katika kuibua kero zinazowakumba wananchi, ili kuona Mkoa wao unabaki salama.

Nao wandishi wa habari waliahidi kuwa waadilifu wakati wanapoandika habari zao, sambamba na kuandika habari zinazoleta mafanikio.

MWISHO.
 
Waandike mema aliyofanya rais wa Zanzibar vipi kuhusu mabaya?
 
Waandishi wa Habari wametakiwa wasiwe waoga bali waendelee kuandika habari zenye ukweli na zenye kuzingatia maadili, ambazo zitaleta maslahi kwa Umma.

Nasaha hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Zukhra Mgeni Othman wakati akizungumza na wandishi pamoja na wadau wa habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa Vyombo vya habari yaliyofanyika Manispaa Chakechake mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema wandishi wa habari wamekua wakikumbana na vikwazo kadhaa wakati wanapokua katika majukumu yao, hivyo wasiwe waoga wasimame penye ukweli na wili watekwe ama wanyimwe Ithibati?andike habari zitakazoleta maslahi kwa Jamii.

‘’Tunafahamu kwamba mmekua mkipata vitisho ila msitishike isaidieni jamii, ilimradi tu muzingatie miko na maadili yenu,’’alisema.
Aidha aliwataka wandishi hao kuandika mema ambayo yamefanywa na Rais wa Zanzibar, wananchi wayafahamu na waweze kujipatia fursa na kuweza kufaidika nayo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Ofisa Mdhamini wizara ya Habari Adam Abdalla Said aliwasisitiza wandishi wa habari kuumwa nan chi yao kwa kuandika habari zenye maslah ya jamii, na wasishie kuandika habari za matukio tu.

‘’Ndugu zangu wandishi wa habari msishie kuandika habari za viongozi tu, bali ibueni changamoto zinazowakumba wananchi wetu na kuweza kutatuliwa,’’alisisitiza.

Mapema mkuu wa Wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja aliwaasa wandishi wa habari kuepuka kuandika habari za uongo, ambazo zitasababisha mifarakano na migongano Nchini.

‘’Siku zote jambo la uongo halina mwisho mwema, hivyo niwatake wandishi wa habari kufanya uchunguzi wa kina juu ya habari watakayoiandika, ili mwisho wa siku ikajakupelekea machafuko na kukosekana kwa amani tuliyonayo Nchini mwetu,’’aliwanasihi.

Mwenyekiti mstaafu wa Jumuia ya Wandishi wa Habari Pemba Press Club (ppc) Siad Mohammed Ali alisema Wandishi wa ahabri ndio sauti ya wanyonge hivyo ipo haja kujikita zaidi vijijini kuibua kero zilizoko ili jamii iishi ikiwa salama.

‘’Wandishi tumesahau wajibu wetu hatuendi vijijini tukasikiliza changamoto, tunaishia kujipendekeza kwa watu wenye uwezo wao,’’alisema.

Mratibu wa Shirika la Utangazaji Ofisi ya Pemba Selme Mohamed Suleiman ili wandishi wa habari waweze kufikia lengo la kuleta mabadiliko katika jamii, ni budi wawe na mashirikiano ya pamoja wakati wakiwa katika kazi zao.

Akiwasilisha mada Katibu wa Jumuia ya Wandishi wa Habari PPC Ali Mbarouk Omar alisema lengo la wandishi wa habari sio kuichafua serikali ni kuandika habari zenye uzalendo na zenye kuleta maslahi kwa jamii na Taifa kiujumla.

Nae Mrakibu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Pemba Aloyce Jakob alisema watahakikisha wanashirikiana na wandishi wa habari katika kuibua kero zinazowakumba wananchi, ili kuona Mkoa wao unabaki salama.

Nao wandishi wa habari waliahidi kuwa waadilifu wakati wanapoandika habari zao, sambamba na kuandika habari zinazoleta mafanikio.

MWISHO.
Ili watekwe ama wanyimwe ithibati?
 
Mimi ni mwanahabari.
Nauliza ni kweli Samia alichaguliwa kwa kura asilimia 98.? Alikuwa maarufu kama kikwete na JPM hapo kabla?
Siulizi kwa ubaya
 
Back
Top Bottom