Pre GE2025 DC wa Kisarawe, Petro Magoti achangia Mifuko 300 ya Saruji Ujenzi wa bweli la Msikiti, ahimiza na wengine wachangie ili Watoto Warudi mapema kusoma

Pre GE2025 DC wa Kisarawe, Petro Magoti achangia Mifuko 300 ya Saruji Ujenzi wa bweli la Msikiti, ahimiza na wengine wachangie ili Watoto Warudi mapema kusoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti ametoa mifuko ya saruji 300 akianza kutanguliza mifuko 150 kwa ajili ya ujenzi wa bweni (hosteli) litakalotumika kwa ajili ya Watoto wanaopata mafunzo ya Dini ya Kiislamu Wilayani hapo ikiwa ni siku mbili tangu alipotoa maelekezo ya kusitishwa kulaza Watoto Msikitini hapo kutokana na mazingira kutokuwa rafiki ya kufundishia na kulaza watoto.
View attachment 3041341
Mifuko 150 imetolewa kwa Msikiti wa FALAF na Mifuko mingine 150 imetolewa kwa Msikiti wa Abdul-Aziz-Asharqiy, kwaajili ya Mabweni ili Watoto wasomee mazingira mazuri ambapo Misikiti yote ipo Kiluvya Madukani Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani

DC Magoti alifika eneo la tukio akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na kukuta Watoto 96 wapo kituoni hapo na kumuelekeza Sheikh wa Msikiti kusitisha huduma hiyo na kuagiza Watoto hao warejeshwe kwenye famili zao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, DC Magoti amesema:

Lengo kubwa la Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwa kila shughuli lazima tushirikishe viongozi wa dini, mimi nikiwa Msaidizi wake ngazi ya Wilaya, tulipopata taarifa kuhusu uwepo wa mazingira haya ambayo sio mazuri tukaona tuwatoe ili ufanyike utaratibu mzuri ili kuboresha mazingira.

Ikiwa Serikali inaweza kujenga miundombinu ya gharama kubwa kwa nini tushindwe kujenga hosteli nzuri na ya kisasa kwa faida ya Watoto wetu!

Baada ya kutoa maelekezo ya Watoto kuondolewa pale, kesho yake nilirejea eneo la tukio Usiku wa Saa Nne nikakuta utekelezaji umefanyika wa kuwaondoa Watoto hao.

Mimi naheshimu sana dini, natambua ndio inaleta upendo, mshikamano na viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa sana.

Kwa leo kwa kuanzia, nimeleta mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa hosteli.

Wale wanaotaka kutuchonganisha tuwakemee na kuwataka nao waje kuchangia ili Ujenzi uishe mapema watoto waendelee na Masomo.

Mimi kama mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama ni jukumu langu kuangalia usalama wa Watu wote wa Kisarawe.

Niwaombe, lengo lenu ni zuri lakini twendeni kwa haraka ili tujenge hosteli ya kisasa na itakayokuwa na mazingira bora.

Pia soma: Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Hawajamshambulia kama aliposema watoto warudi makwao
 
Back
Top Bottom