DC wa Korogwe Jokate punguza Sifa na Kiherehere zitakuja Kukuponza

DC wa Korogwe Jokate punguza Sifa na Kiherehere zitakuja Kukuponza

Lakini huyu ndiye DC anaye shine kila wilaya anayopangiwa. Naona unamtolea povu jingi na kali. Huenda hizi mbio zitaingiza fedha nyingi kuweza kutimiza lengo lake. Mbona kuna wanawake ambao wana nguvu nyingi kufanya kazi ngumu mpaka tarehe ya kujifungua, kuna wengine hukimbia huku wakiwa na mimba zao kiasi cha kuwaonea huruma wasisumbue kiumbe kilichopo tumboni. Anyway, huyu ndiye dc mbunifu kuliko ma dc wote
Mfano anefabya kitu gani Cha maana hadi sasa kwenye ukuu wa wilaya?
 
Jokate Kama Moshi vile huwezi zuia na mikono......hata apelekwe Hadzabe district atagundua tu Jambo la kuwapa Wanahabari kazi ya kufanya
 
Ila ndugu ujinga tafsiri yake ni kuto kuwa waelevu, sasa siyo waelevu kwa lipi.

Maana tusije jikuta sisi ndiyo wajinga, kwa kuto tumia neno ujinga sehemu sahihi.
Mjinga ni yeyote anayeweza jifunza
 
Je daktari ameshauri kufanyika hivyo?

Kila mama Mjamzito anapaswa kuhudumiwa separately sio jumla jumla.

Wengine ukute wanaumwa presha Na hawajijui sababu wengine hata early and regular clinic hawafanyi hadi akaribie kujifungua,

Kwa hiyo kumkimbiza Mjamzito au kumtembeza mwendo mrefu ni hatari vinginevyo ishauriwe na daktari.
 
Angeshirikiana na mabwana afya kukagua vyoo kwenye makazi na stand za mabasi kisha kuhamasisha kujenga vyoo vya kisasa vyenye gharama nafuu ningemuelewa.

Hii natamani ingefanyika kila mahali nchi hii.
 
Back
Top Bottom