DC wa Serengeti atoa siku 7 kwa wanasiasa waliowadanganya wafanyabiashara

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dkt. Vicent Mashinji ametoa siku 7 kwa viongozi wa siasa waliowaambia wafanyabiashara warejee katika maeneo yao ya awali ya biashara na kuondoka katika maeneo yaliyotengwa, kwenda kukanusha kauli zao vinginevyo atawachukulia hatua kali za kisheria.

“Niwaagize wote mliokuwa mmeenda kutoa kauli hizo (wafanyabiashara kurejea kwenye maeneo ya awali) nendeni mkazikanushe haraka kabla hatua kali hatujawachukulia.

“Haiwezekani wananchi tunawawekea eneo maalum ninyi mnaenda kupotosha,“ - Dkt. Vicent Mashinji.


Chanzo: Dar Mpya
 
Sukuma Gang wameanza kuweweseka baada ya CCM ya zamani kurejea.
 
Huyu mpuuzi naye ni DC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…