DC wa Tarime, Meja Gowele: Mwananchi anayepata changamoto Kituo cha Afya Nyangoto atoe taarifa mapema

DC wa Tarime, Meja Gowele: Mwananchi anayepata changamoto Kituo cha Afya Nyangoto atoe taarifa mapema

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele amefanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Afya Nyangoto, kinapatikana Nyamongo Mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime Vijijini, Kata ya Matongo ambapo amezungumza na Wagonja na uongozi wa kituo hicho.

Ziara hiyo imefanyika baada ya Mdau kuelezea changamoto kadhaa alizodai zipo katika kituo hicho ikiwemo Wamama Wajawazito kutozwa Tsh. 3,000 kila anapohudhuria kliniki na Tsh. 3,000 kwa wale wanaoanza wakati maelekezo ya Serikali ni kwamba Wajawazito wanapata huduma bure.

Mdau alieleza kwamba Watumishi wa kituo hicho hawatoi risiti, na kwa wale wanaofanya mchakato wa kupima damu maabara wanapokea fedha na kuziweka mfukoni, pia akadai Kadi za Kliniki zinazotolewa ni za ‘photocopy’ na siyo kadi original.

Hoja ya Mdau ~ Wajawazito wanalipia huduma Kituo cha Afya Nyangoto na hawapewi risiti, kadi za Kliniki wanapewa za photocopy sio original

DC Gowele amesema “Nawapongeza Watoa huduma, najua kuna changamoto ndogondogo zipo kwa baadhi ya wanaoamua kuchafua, nao tutahangaika nao, tunahitaji wananchi wapate huduma bora, kuna watu wanakuja kutoka nje ya nchi kupata huduma hapa, waje wayakute hayo kwa sababu ya mtumishi mmoja? Tutahangaika naye.”

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ni Dkt. Amin Vasomana alikuwa na haya ya kusema;


 
Back
Top Bottom