DCP Mambosasa: Ni kosa kumkamata asiyehusika wakati wa kumtafuta mtuhumiwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Dkt. Lazaro Mambosasa, ametoa rai kwa askari wa Jeshi la Polisi nchini kuacha tabia ya kukamata raia wasiohusika ili walisaidie jeshi kumtafuta mtuhumiwa.

Akizungumza katika mahojiano na TBC Digital chuoni hapo, Dkt. Mambosasa ametolea mfano wa polisi kumkamata mke wa mtu ili kumpata mume wake mtuhumiwa, akisema kwamba hatua hiyo inakiuka sheria na haki za raia ambao hawana kosa, na mara nyingi husababisha kuingia kwenye migogoro.

Aidha, amewashauri Watanzania kuwa wakishakutana na vitendo hivyo vya askari, wahakikishe wanaripoti au kutoa taarifa ili haki za raia zisivunjwe.

Kwa hali ilivyochafuka, ningewaona mnamaanisha kama mngesema mmewafanya nini waliofunja huo utaratibu.

Maneno tu, maneno tu yanasaidia nini
 
Umekamatwa na police kimakosa je utaenda kutoa taarifa wapi bwana mkuu?
 
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Dkt. Lazaro Mambosasa, ametoa rai kwa askari wa Jeshi la Polisi nchini kuacha tabia ya kukamata raia wasiohusika ili walisaidie jeshi kumtafuta mtuhumiwa.

Akizungumza katika mahojiano na TBC Digital chuoni hapo, Dkt. Mambosasa ametolea mfano wa polisi kumkamata mke wa mtu ili kumpata mume wake mtuhumiwa, akisema kwamba hatua hiyo inakiuka sheria na haki za raia ambao hawana kosa, na mara nyingi husababisha kuingia kwenye migogoro.

Aidha, amewashauri Watanzania kuwa wakishakutana na vitendo hivyo vya askari, wahakikishe wanaripoti au kutoa taarifa ili haki za raia zisivunjwe.

Wana kipaji cha utapeli. Maneno matupu.

Kwanini wasianze na kuwawajibisha Polisi/vyombo vya usalama waliomkamata dada yake na Polepole na kumpiga vibao wakati wakimtafuta Polepole?
 
Afande Mambosasa ni PhD holder kwa sasa, ndio maana anatoa hoja za kisomi.
 
Back
Top Bottom